Mbinu Mpya Ya Kupata Kazi Ukihitimu Chuo

Mbinu Mpya Ya Kupata Kazi Ukihitimu Chuo

Soko la ajira ni changamoto kubwa inayosumbua vichwa vya wanafunzi wengi hasa wale wanaohitimu vyuo vikuu katika nyakati hizi. Jambo ambalo linafanya vijana wengi wakose imani ya kufanikiwa tena.

Kwanza ijulikane kuwa degree peke yake sio kigezo cha mhitimu kupata kazi kwa sababu wengi huamini akimaliza chuo kazi ni yake japo kwa sasa vijana wameanza kulielewa soko. Kipindi tulichonacho ni kipindi ambacho bila kujiandaa mapema mambo huwa ni magumu sana huko mbeleni, soko la ajira ni gumu.

Mfano TRA walitangaza nafasi za kazi wakitaka watu 1,596 lakini waliojitokeza kuomba nafasi hizo ni 135,027 maana yake watu takribani watu 133,431 walikosa hiyo kazi. Jaribu kufikiria ni kwa jinsi gani wasomi walivyo wengi mtaani na hawa wote wanazisaka hizo kazi.

Ndio maana nasema ni bora kujiandaa mapema wakati bado upo chuo bado huna mambo mengi ya kushughulika nayo.

Hata hivyo, kupenya kwenye soko la ajira ni jambo linalohitaji juhudi, ujuzi na utayari wa mtu mwenyewe. Katika makala hii, tutaangazia jinsi mwanachuo anavyoweza kupenyeza kwenye soko la ajira.

Je, ni nini unachoweza kufanya kama mwanachuo ili kuongeza uwezekano wa kupata kazi?

Mchakato wa kutafuta kazi unapaswa uanze mapema, hata kabla ya kuhitimu. Je wewe ni mwanachuo?

Kama jibu ni Ndiyo, basi unaweza kuanza kutafuta fursa za kazi mapema mtandaoni au kwa kushiriki katika programu, miradi, semina mabli mbali ili upate exposure ya kukutana na watu walioko kwenye field unayoisomea, kuandaa projects ambazo utakuwa unaonyesha watu utakakuwa unakutana nao.

Vile vile angalia na tenga muda vizuri tafuta makampuni yaliyopo karibu uanze kujitolea. Hii itakufanya ukutane na watu ambao yamkini watakuja kuwa daraja zuri kupata kazi pindi tu unapomaliza chuo.

Pia ukianza kujitolea mapema ukiwa chuo utapata uzoefu wa kazi mapema through internship/freelancing ambao utakusaidia kuwa na ujuzi unaohitajika kwenye hili soko letu la ajira.

Ivi ulishawahi kusikia au kuulizwa hili swali, unauzoefu wa miaka mingapi? chukulia ndio tu umemaliza chuo halafu unaingia interview unaulizwa hilo swali, utajibu nini? Hivyo anza mapema kutafuta makampuni ujitolee wakati bado upo chuo atleast utakuwa unauelewa wa hapa na pale.

Soko la ajira linataka nini?

Kwa kuwa dunia inaenda kwa kasi sana kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kitu muhimu kinachohitajika zaidi ni mtu mwenyewe kuwa tayari kuendelea kujifunza kila siku.

Kuwa tayari kuitumia mitandao ya kijamii kujenga uhusiano mzuri na watu lakini pia kutafuta fursa za kazi mbali mbali. Siku hizi hata ukiwa unafahamu mambo kiasi gani kama watu hawakuoni, hawaoni hayo maarifa uliyonayo ni ngumu kupata fursa.

Lazima uonyeshe kile unachokijua ndipo watu watakufuata wakupe kazi.

Muhimu: Kwa dunia tuliyopo, kama mwanachuo ataamua kuitumia vizuri mitandao ya kijamii yaani social media platforms kama Linkedin katika kujiuza (personal branding) basi mtu huyu;

Hatakuwa anatafuta kazi bali kazi zitakuwa zinamtafuta yeye by Shukuru Amos.

Soko linahitaji vijana wenye maarifa ya kufanya kazi fulani, kuna kazi zingine hata hazihitaji cheti kikubwa uwe na uwezo wa kutatua changamoto za kampuni husika au uwezo wa kuisadia kampuni ikaongeza mauzo au kupandisha hadhi yake?

Jinsi gani unaweza kuboresha ujuzi wako, kupata maarifa yanayohitajika katika tasnia uliyopo?

Technolojia inabadilika kwa kasi sana hivyo unaweza kutumia mitandao ya kijamii kufuatilia mabadiliko yanayotokea katika tasnia yako na kujifunza ujuzi mpya kupitia kozi mbalimbali mtandaoni ikiwemo Marketing.

Chuoni utapewa Mwongozo tu hivyo kuna kila sababu za kutafuta maarifa zaidi. “Kama elimu ya chuo itashindwa kukufanya kuwa unachotaka basi Professor Youtube na msaidizi wake Google wanaweza”.

Utajiuliza ni kivipi Youtube au google inaweza kukusaidia kutimiza ndoto zako? Unahitaji tu kujua unataka usome nini then weka bundle YouTube anakufungulia dunia kuwa unachotaka.

Je ni sahihi kuweka wasifu wako mtandaoni?

Kutengeneza wasifu wako mtandaoni kunaweza kukusaidia sana katika harakati za kutafuta kazi. Wasifu huo utakuwa hewani 24/7 unasomwa na watu wa aina tofauti tofauti ikiwemo waajiri wako baadae, wateja wako.

Hivyo ni vyema kuweka mawasiliano yako, barua pepe na nambari ya simu katika kurasa zako ili watu wakikuhitaji iwe rahisi kukupata.

Wasifu wako mtandaoni unaweza kuwa fursa nzuri kwa wateja au waajiri wanaotafuta talents mtandaoni kujua zaidi kuhusu wewe, uwezo wako na kitu unachoweza kuwasaidia.

Iwe ni Twiter, Facebook, au LinkedIn we jiweke as a professional wa kitu fulani huwezi kujua huko mbeleni ni fursa gani unaweza kuipata. Who knows what will happen tomorrow?

Nifanye nini ili nitambulike na niweze kupata kazi?

Kujitangaza ni muhimu sana katika ulimwengu wa kidigitali hasa unapokuwa kwenye harakati za kutafuta kazi.

Wewe Mwanachuo unapaswa kuwa na ujuzi wa kujielezea mwenyewe katika majukwaa ya aina yoyote iwe kwa maandishi au kwa kuongea.

Kujifunza jinsi ya kuwa mbele kiujuzi na kimaarifa kunaweza kukusaidia kuwa na ujasiri, uwezo wa kuwasilisha mawazo, kushawishi waajiri wakupe kazi.

Asilimia 90 ya mazungumzo mtandaoni huwa ni kwenye maandishi hivyo ni bora kuwa vizuri zaidi kwenye uandishi.

Bonus: Mtu awaye yote, mwenye kutafuta afueni ya maisha yake, yambidi afanye bidii na juhudi zote katika kutatua matatizo yanayoisibu tasnia yake.

Nimalizie kwa kusema tatizo la ajira halitakaa liishe bali litaongezeka maradufu.

Je, ChatGPT Inaweza Kudukua Taarifa Zako?

Je, ChatGPT Inaweza Kudukua Taarifa Zako?

Hapana. ChatGPT haiwezi kudukua taarifa za watumiaji wake. Zana hii ya AI (Artficial Intelligent) ipo kwa lengo la kukusaidia kufanya kazi zako kama vile kuandaa maudhui kwa uharaka na ufanisi mkubwa.  

Pia ChatGPT, amabaye kimsing ni roboti unayeweza kufanya mazungumzo naye, anaweza kukupatia majibu ya maswali yako yoyote utakyouliza.

Hizo ndizo kazi za ChatGPT. Siyo kukusanya au kudukua taarifa zako.

Kama ulishawahi kutumia ChatGPT utajiuliza kwanini upande wa kushoto mwa smartphone au desktop yako ukiwa ume-login huwa kuna record za maswali yote uliyokwisha kumuuliza ChatGPT?  

Ni kwamba mazugumuzo yote ambayo unafanya na ChatGPT hurekodiwa kwenye (hifadhidata) database ya OpenAI. Hii inakuwezesha wewe kuweza kuona mambo yote uliyowahi kuchati naye. Lakini pia inakupa option ya Ku-delete kama huhitaji mazungumzo yaendelee tena kuligana na mada uliyokuwa unachat naye.

Pia huisaidia ChatGPT kukumbuka nini mnazungumzia hasa mazungumzo yakiwa ni endelevu.  Hapo tunapata hili Swali hapa chini:

Endapo hifadhidata ya OpenAI itakuwa-attacked, je, taarifa za mtu zinaweza kudukuliwa?

Hilo liko wazi; kama uliwahi kutoa taarifa zako binafsi (sensitive data) kwa ChatGPT basi hautakuwa katika mikono salama tena katika kipindi ambacho hifadhidata ya OpenAI itakuwa attacked.

Steve Mills, mtaalamu wa masuala yahusuyo AI na Maadili anasema “then you have lost control of that data and somebody else have it.” Ndio maana unaambiwa usimshirikishe ChatGPT taarifa zako binafsi.

Fuatilia katika hii link https://www.openai.com/blog/march-20-chatgpt-outage

Je, matumizi ya ChatGPT yanaweza kusababisha kuvuja kwa taarifa za kampuni?

Ndiyo, kama kuna mmoja kati ya wafanya kazi katika kampuni anatumia ChatGPT katika shughuli zake na kwa namna moja ama nyingine alihusisha au huhusisha taarifa nyeti za kampuni pindi akiwa anawasiliana na ChatGPT, Mtu huyu anaweza kusababisha security breaches of the network endapo tu akaunti yake ya ChatGPT itakuwa hashed/known na kuwapa uwanda mpana watu wengine kupata network datails alizoshare na ChatGPT akiwa anachat.

Hapa kwenye hashing itategemeana na urefu, ugumu wa nenosiri, kifaa anachotumia n.k.  Kumbuka hapo pia kuna Man in the middle attack.

Samsung waliliona hili na hivyo kuzuia wafanyakazi wake wasitumia generative AI kama ChatGPT ili kulinda usalama wa kampuni.

Jinsi ya Kutumia ChatGPT Kuandaa Maudhui (Content Creation)

Jinsi ya Kutumia ChatGPT Kuandaa Maudhui (Content Creation)

Kama huna jeshi la maroboti mtandaoni yanayo kufanyia kazi masaa 24, basi wewe haujaingia rasmi kwenye ulimwengu wa digitali. You are not digitally savvy enough.

Maroboti haya (bots) inaweza kuwa tovuti uliyoiandaa vyema kweye SEO kiasi inajionyesha kwa watu wakitafuta huduma unayotoa. Zana (tools) zinazokusaidia kufanya research, n.k. ChatGPT ni moja kati ya roboti za mtandaoni anayeweza kukusaidia kufanya mambo kibao.

Kabla hatujaenda mbali, naomba kuweka wazi jambo moja:  ufanisi wa zana yoyote, iwe ChatGPT au jembe la mkono, unategemea na mtu anayoitumia zana hiyo. Hivyo wapo watakao faidika na ChatGPT na wengine hawatafaidika.

So ChatGPT ni nini?

Ni software/roboti mwenye uwezo kiufahamu na kufikiri unaofanana na binadamu (Artificial Intelligence). Unaweza kupiga naye stori mbalimbali.Anaweza kujibu swali lolote. Unaweza kumwambia akuandikie chochote kama vile insha, kutunga wimbo na mambo mengine kibao.

ChatGPT anaweza kukusaidia kwenye maswala ya kukuandaa maudhui. Kama huwa unaumiza kichwa juu ya nini cha kupost mtandaoni, basi umepata mkombozi.

Jinsi ya Kutumia ChatGPT

Ni rahisi sana. Ni kama vile unachat na mtu kwenye WhattsApp. ChatGPT anapatikana kwenye kifaa chochote, smatphone au laptop.

Hatua ya kwenza nenda kwenye hii tovuti,  https://chat.openai.com/chat

Hapo utaombwa ku-login au ku-sign up kama bado huna akaunti.

Baada ya hapo anza kwa kuuliza chochote. Kumbuka, japokuwa ChatGPT anaweza kuzungumza Kiswahili, yuko vizuri zaidi kwenye Kiingereza. Kwenye Kiswahili wewe unamzidi so usihangaike kuuliza maswali ya Kiswahili.

Kuandaa Maudhui na ChatGPT

Kama unapata shida juu ya nini cha kupost linkedin, twitter, au kwenye blog na kurasa zingine za website yako, basi ChatGPT atakuwa msaada mkubwa kwako. Inabidi uwe vizuri katika kumpa maelekezo ili akupatia kile unachotaka. Maelekezo mabovU maana yake utapata matokeo mabovu.

Tuseme wewe ni mtu wa Finance na una CPA yako vizuri tu. So unataka kuwa miongoni mwa watu wanaozungumza juu ya maswala ya finance. Lengo likiwa ni kutengeneza jina na pengina kujipatia fursa za ajira

Hebu tumuulize ChatGPT tupate pa kuanzia

What topic do finance people talk about on linkedin?

Haya sasa umeshapata mada za kuongelea. Unaweza kuchukua hizi mada na kuziandikia jambo mwenyewe unaweza kurudi tena kwa ChatGPT.

Tuchukue hicho kipengele cha tatu kwenye picha “Personal finance and financial planning” halafu tumwambie ChatGPT atengeneze linkedin post;

Hapa picha nimeikata alivyoandika huko chini. But you get the point.

Jinsi unavyo kuwa SPECIFIC kwenye maelezo ndivyo ChatGPT  atakupatia majibu mazuri

Mfano wewe si mtu wa Finance tu aliye kwenye entry level career bali ni finance exacative mwenye lengo la kujenga thought leadership miongoni mwa wakurugenzi na young finance professionals. Basi unaweza kuwa SPECIFIC kwa kuuliza:

I am a finace executive who want to build thought leadership among senior executives and young finance professionals on LinkedIn. What topics or issues I should be talking about?

Au kama upo kwenye digital marketing, umejikita kwenye nini?  Usimpe chart maswali ya mjumuisho. Kama upo kwenye SEO, au Copwriting basi uliza mwasali kwenye hizo topic na si mwaswali general digital marketing.

Kumbuka sio post za linkdine tu, unaweza kuandika chochote kupitia ChatGPT. Mfano kama unataka kuandika makala mpya kwenye blog yako utasema;

Write a 500 words blog article about 5 easiest online businesses to start in 2023.

Mfano wa kuwa SPECIFIC

Nilimuomba ChatGPT aniandikie maneno yenye kushawishi ili niweke kwenye landing page ya website yangu. Haya ndiyo maelekezo nilimpa:

I am a Copywriter and content strategist helping Business founders, C-suites, and Freelancers to build online audiences, engage with insights and build thought leadership. 

I want you to create copy for my landing page. 

The H1 title is this: Get what you want through mastering impactful delivery.

Tell them that I Coach them to communicate and engage with insights on social media. Equip them with the method and tools of impactful delivery. 

They will then build authority and have the confidence to attract and convert clients.

Make an insist that everyone they see online is an expert in something. What they don't have in common, which is something I will give them through my service, is that not all of them are good online communicators who can get what they want through the power of words.

Please address them directly. Use the pronoun you.

ChatGPT hakuwa mchoyo, aliniandikia hiki 👇🏼 ambacho siyo mbaya.

“Are you ready to take your online presence to the next level? 

As a business founder, C-suite executive, or freelancer, you have the expertise and knowledge to make a real impact. But not everyone you see online is a master of impactful delivery.

That's where I come in. As a copywriter and content strategist, I'll coach you to communicate and engage with insights on social media. I'll equip you with the methods and tools to deliver your message with power and persuasion. And with my guidance, you'll build authority and confidence, attracting and converting clients with ease.

Don't let your message fall flat. Master the art of impactful delivery with my coaching and see the results for yourself. Get what you want through mastering impactful delivery with me."

Usisahau Kuhariri

Kama ulivyoona, kuna haja ya ku-edit alichoandika ChatGPT. Itabidi uongezee au kuondoa vitu. Hakikisha unasoma na kuona kama kilichoandikwa kina-make sense.

Kumbuka

Tumia ChatGPT kuongeza ufanisi kwenye kazi yako. Maana yake wewe mwenyewe tayari uko vizuri na si unakuwa tegemezi kwenye hiki kifaa. 

Ubora wa matokeo utakayoyapata kutoka kwa ChatGPT unatokana na ubora wa maelezo utakayo mpatia kama. Kama lugha ya kiingereza inakusumbua basi utapata changamoto kutumia ChatGPT.

Asante kwa kusoma mwongozo huu.

Naitwa Shukuru, ninaandika kuhusu kujiajiri kwenye uchumi wa digitali pamoja na jinsi ya kuuza mtandaoni. Nifollow LinkedIn kwa jina la Shukuru Amos.

Jinsi Ya Kumsaidia Mjasiriamali Mdogo Kukuza Biashara Yake Mtandaoni

Jinsi Ya Kumsaidia Mjasiriamali Mdogo Kukuza Biashara Yake Mtandaoni

Hakuna mtu ambaye anaweza kufanikisha jambo bila msaada wa mtu au watu wengine. Tunaishi kwa kutegemeana. Unachokitafuta wewe kipo kwa mtu mwingine.

Katika dunia yetu ya kidigitali, ni rahisi kuwa sehemu ya msaada mkubwa kwa wajasiriamali wanaotafuta kukuza biashara zao mtandaoni. Unaweza kufanya hivyo bila hata ya kutumia pesa.

Jinsi ya kusaidia kukuza biashara ya mjasiriamali mtandaoni

Follow page yake ya biashara. Inaweza kuwa ni instagram, twitter au facebook - popote unapoona unaweza kumfolllow fanya hivyo. Hii haigarimu pesa yoyote.

Toa Comment , Like au Share post za bidhaa zake ili zipate kuonekana kwa wengi. Kumbuka wewe binafsi una followers ambao nao wana followers, hivyo ukishare au kucomment kweny post ya mjasiriamali huyu, unaipa nafasi post yake kufika mbali zaidi. Hii nayo haikugarimu hela.

Toa maoni, reviews auratings kuhusu huduma yake kwenye page yake Google My Business, kwenye App yake playstore, au kwenye listing directories zingine.

Weka picha ya eneo au bidhaa yake na shiriki kuhakiki (verify) taarifa zake kwenye ramani za google.

Pia wajuze marafiki zako juu ya bidhaa zake.

Cha mwisho, acha kuponda biashara ya mtu mtandaoni. Kama kuna kitu unaona anakosea ni busara kumtumia ujumbe inbox na kumweleza.

Ukifanya yote haya, utakuwa umetumia kiasi cha shilingi SIFURI!

Lakini utakua umemwezesha mtu kufikisha bidhaa yake kwa walengwa hivyo kujipatia kipato cha kuendesha maisha yake. Si lazima uwe na pesa kusaidia, japo ni vizuri zaidi kutoa ukiwa na uwezo huo.

Kama somo limeeleweka, naomba follow page za Tanzlite Digital kwenye mtandao wa LinkedIn, Facebook, Twitter na Instagram. Pia nenda kafanye hivo kwenye biashara ya mjasiriamali unayemjua.

Kugusa maisha ya watu wengine si lazima uwe Bill Gates. Kusaidia kukuza online visibility ya biashara ya mtu ni aina nyingine ya philanthropy!. Tuendelee kuinuana. Usisahau kushare post hii 🙂

Natumaini makala hii imekusaidia. Naitwa Shukuru, ni mwandishi na mtaalamu wa Digital Marketing. Nipate kupitia mtandao wa WhatsApp hapa.

Fahamu Makundi Matatu ya Wateja Mtandaoni (na Jinsi ya Kuwapata)

Fahamu Makundi Matatu ya Wateja Mtandaoni (na Jinsi ya Kuwapata)

Idadi ya Watanzania wanaotumia internet imefikia milioni 27. Katika mamilioni haya ya watu, kuna wateja wengi sana kwa ajili ya biashara yako. Lakini UNAWAPATAJE? Au wanakupataje? 🤔

Kabla hujaanza kutumia njia yoyote ya kidigitali kupata wateja mtandaoni, ni vyema ukafahamu makundi matatu ya wateja wanaopatikana mtandaoni. Itakusaidia kuandaa mpango (digital strategy) utakaoleta matokeo mazuri.

Makundi Matatu ya Wateja Mtandaoni 

1.Wateja wanao kufahamu: hawa ni wale ambao tayari wanajua biashara yako. Wanaweza kuwa ni followers kwenye account zako za mitandao ya kijamii, au una email list yao au wame-subacribe kupata huduma yako. 

Hawa ni rahisi kuwauzia bidhaa yako. Watu wakikufollow ujue tayari wamevutiwa na unachokifanya. 

Kazi yako ni kuwapa huduma bora ili wakakutangaze kwa wenzao. Fanya kila uwezalo kuhakikisha hili kundi haliondoki (Customer Retention

2. Kundi la pili ni wateja wanaohitaji bidhaa yako lakini hawakujui. Hawa wanaweza kuwa wanapata bidhaa hiyo kutoka kwa mtu mwingine au hawajui wapi pa kuipata. 

Kama wanaipata bidhaa hiyo kutoka kwa mtu mwingine maana yake tayari una mshindani. Hapa unakuwa na kazi ya ziada ya kumchunguza mshindani wako. Anatumia mbinu gani kupata wateja na bidhaa yake ni bora kiasi gani kulinganisha na yakwako. 

Je anatumia influencers? Maudhui yake ni bora kiasi gani? Ni mtandao gani wa kijamii amejikita zaidi? Ukifahamu haya na mengine utaweza kuja na mkakati (digital strategy) imara wa kukuza biashara yako. 

Kwa kuwa kundi hili ni la watu wenye UELEWA juu ya wanachohitaji, wengi hutumia search engines kutafuta bidhaa hiyo (they are actively searching online). Hivyo njia nyingine ya kuwapata ni kuwa na mpango imara wa SEO (Search Engine Optimization) au kutumia matangazo ya Google Ads

3.Kundi la tatu ni la wale ambao wangependa kutumia bidhaa yako lakini hawajui kama wanahitaji (they don't know if they need it). Hapa sasa inabidi uwe vizuri kwenye kitu tunaita Content Marketing. Kundi hili la wateja wanahitaji kuelimishwa sana kabla hawajafanya maamuzi ya kutoa hela yao kununua huduma yako. Wanahitaji elimu juu ya tatizo walilo nalo na kwamba kuna suluhu ya tatizo hilo ambayo ni hiyo bidhaa yako. 

Mara nyingi ukiwa umegundua solution mpya juu ya tatizo fulani, tuseme ni software, tiba lishe au kitu chochote —watumiaji wa solution yako mara nyingi wanakuwa kwenye hili kundi la tatu. Wanahitaji maudhui ya kutosha kuwafundisha tatizo lililopo, madhara ya tatizo hilo na faida za kutumia bidhaa yako. 

Hitimisho

Kumbuka biashara ni watu. Kufahamu makundi ya wateja na tabia zao mtandaoni itakusaidia kuandaa mpango wa digitali wenye kuleta mafanikio katika biashara yako. Hasa upande wa maudhui kwani makundi haya matatu yanahitaji aina tofauti ya maudhui.

Ukiwapa huduma bora wateja waliopo kwenye kundi la kwanza hapo juu, wanaweza kuwa mabalozi wazuri kwa wateja wa kundi la pili na la tatu.

Natumaini makala hii imekusaidia. Naitwa Shukuru, ni mwandishi na mtaalamu wa Digital Marketing. Nipate kupitia mtandao wa WhatsApp hapa. Au jiunge na group letu la Wafanyabiashara wadogo mtandaoni kwa Tsh 7500.

Jinsi ya Kupata Wateja Mtandaoni Kupitia Matangazo Mguso (PPC Advertising)

Jinsi ya Kupata Wateja Mtandaoni Kupitia Matangazo Mguso (PPC Advertising)

Kukua kwa matumizi ya internet nchini Tanzania kumerahisha uwezekano kukuza biashara yako na kufikia wateja wengi mtandaoni. Zipo njia nyingi za kuweka biashara yako kwenye mtandao ikiwemo tovuti, mitandao ya kijamii, kupitia WhatsApp, email na nyingine nyingi.

Katika zama hizi za digitali, watu hufanya utafiti wa bidhaa wanayotaka kununua kabla ya kufanya maamuzi ya kununua. Utafiti wao mwingi unahusisha kutafuta (Search - au kugugo) kwenye injini za utafutaji pamoja na kusikiliza ushauri wa watu ambao wamewahi kutumia bidhaa hiyo.

Kwa wenye biashara zenye website, ipo njia ya kunasa wateja kwa haraka. Njia hii ni kutumia matangazo mguso (PPC ads). Njia hii huitaji kusubiri miezi kadhaa kuanza kupata watembeleaji kwenye tovuti yako kama ilivyo  kwenye mpango wa SEO.

Ukiwa mfanyabiashara, kuonekana kwenye matokeo ya utafutaji (search results) ni fursa kubwa ya kutangaza bidhaa au biashara yako ili watumiaji hawa wa mtandao (internet) waweze kuona biashara yako. 

Maana yake kama hauko online, watafutaji hawa watakukosa na mshindani wako aliyeko online atapata fursa ya kunasa hawa wateja.

 

Injini za utafutaji kama vile Bing, Google na Yahoo zina huduma ya kuweka matangazo kwenye matokeo ya utafutaji (search results) 

Kitaalamu inaitwa Paid Per Click Advertising (PPC). Ni aina ya kutangaza bidhaa au huduma kwa kununua maneno maalum (keywords) yanayohusu biasha yako ambapo utaweza kuonekana endapo mtumiaji akitafuta kwa kutumia maneno hayo. Maana ya jina Pay Per Click ni kwamba unalipa endapo mtu atabofya tangazo lako na kuzuru tovuti yako.

Matangazo haya hukaa mwanzoni mwa ukurasa wa matokeo ya utafutaji (search engine result page), yakifuatiwa na matokeo ya kawaida (organic results). Pia yanaweza kuonekana sehemu nyingine ndani ya results page.

Tazama picha ifuatayo:

Ufafanuzi kuhusu picha ya juu.

  1. Ni uwanja wa kutafutia (search bar) ambapo mtu ametafuta ‘stuffed animals’
  2. Vertical navigation (hapa unachagua uone matokeo ya Picha, Bidhaa, Video, Maeneo au Habari)
  3. Taarifa kuhusu matokea ya utafutaji (search results information)
  4. Haya ndiyo matangazo mguso (PPC Ads) 

PPC Inafanyaje Kazi? 

Matangazo haya hutolewa kwa ushindani au mnada. Wenye biashara hushindania maneno kwa kuweka dau kubwa juu ya mwenzake ili apate kuonekana  endapo mtu ‘atagugo’  kwa kutumia maneno hayo. 

Hivyo, mambo mawili ni muhimu kuzingatiwa;

  1. Dau lako kulinganisha na dau la mwenzako (auction) 
  2. Ubora na uhalisia wa huduma yako (quality and relevance) 

Hebu tuangalie mfano ili upate kufahamu zaidi:

Tuseme unamiliki hoteli na unataka kutangaza kupitia matangazo mguso. Washindani wako wengine kama kampuni mbili hivi  nazo  zinataka kutangaza. Hapo 

  • Best hotels in Serengeti
  • Serengeti National Park 
  • Tanzania adventures 
  • Best hotels in Tanzania
  • Luxury resorts in Tanzania

Tuseme wote mmechagua maneno hayo juu. Wewe ukaweka dola mbili per click, mshindani wako akaweka dola nne kwa kila mtu atakapo bofya tangazo. Hapa maana yake mwenzako atakuwa anaonekana zaidi kuliko wewe kwenye paid search results

Mara nyingi gharama za malipo per click hupanda kutegemea na ushindani na eneo unalotaka kutangaza. Kwa mfano, wewe ni Hosting company au Insurance company katika jiji la New York, hapo ushindani kwenye keywords utakuwa mkubwa hivyo utalazimika kuweka pesa nyingi.

Lakini kwa nchi kama Tanzania, makampuni mengi hawatumii PPC advertising, hivyo linaweza kuwa chimbo zuri kwako wewe kunasa wateja. Unaweza kujikuta ni wewe tu unayetangaza katika sekta yako.

Lakini pia kuna vigezo vya ubora na uhalisia wa maudhui na jinsi tovuti yako ilivyoundwa. Hivi vinaweza kuathiri uwezekano wa kuonekana kwenye matokeo ya utafutaji. Ikumbukwe lengo la google ni kutoa matokeo sahihi kwa watumiaji wake na kuhakikish user experience ni ya kuridhisha. Hivyo unaweza kuwa na dau dogo kuliko mwenzako lakini bado ukaoneka.

Vipi kuhusu ufanisi wake? 

Ufanisi wa aina hii ya matangazo ni bora zaidi kwasababu hapa unatangaza kwa watu ambao tayari wako interested na biashara yako. Yaani unalenga wateja ambao tayari wanatafuta huduma yako (customers who are actively searching for your product or service). 

Kupata umaarufu (awareness and recogntion) wa biashara yako mtandaoni inachukua muda kutegemea na maarifa na jitihada ulizo wekeza. Lakini kwa kutumia matangazo mguso (PPC) unaweza ukajulikana na kuanza kuvutia wateja kwa muda mfupi sana. Ni jambo la siku au masaa tu. 

Unahitaji kufahamu zaidi au kufanyiwa huduma hii kwenye biashara yako? Wasiliana nasi HAPA