Kuwa makini kuhusu Followers na Engagement unayopata. Kuna mwamba pale LinkedIn anafollowers 155,300+. Ni wengi si ndiyo?
Post zake ni zile za Agree? —si unazipata zile? Yaani mavichekesho, post za huruma na mambo kama hayo.
Likes ni nyingi kupita maelezo. Sometimes zinafika hadi 54,000+ kwa post moja.
Unaweza sema huyu mwamba kashatoboa si ndiyo? From the look of it sidhani. Kwa maana hadhi ya jina lake bado DHAIFU na Hawezi Kuuza. Ana followers. Hana influence.
Huyu akisema auze bidhaa atajikuta anashangaa kama Yesu, “wako wapi wale kenda?” Anaweza asiuze kabisa kwa wasifu ule alionao. Unajua ni kwanini?
Anajitambulisha kama Expert in Digital Marketing lakini watu wanamjua kama jamaa anayepost vitu flani funny au motivating. Hawajui anaweza kuwasaidia nini. Kwasababu ukishuka kwenye post zake, post ya kwanza hadi ya ishirini huoni post kuhusu ujuzi na maarifa yake. Yaani yeye kama yeye hana cha kuongea. Siyo creator. Ni msambazaji wa yale anayokusanya huko mtandaoni.
Akijaribu kupost huduma engegement inaporoka kutoka likes zaidi ya 20,000 hadi likes chini ya 20. Yaani amejikusanyia audience ya watu wenye attention span ya TikTok. Hawa ni kama wale walioponywa ukoma wakaenda kimoja bila kurudi kumshukuru Yesu.
Usiende mtandaoni kukidhi mihemko ya watu. There is what sells on a particular platform, and there’s WHY you are there. If you’re there to entertain the ramblings of incoherent masses then fine.
Usilewe Followers
Penye nzi, fisi na mwewe wengi pana bidhaa ambayo walaji wake wana uwezo (read kipato) mdogo. Yaani hawana uwezo kama simba au chui kukimbiza swala, kumuua na kumla.
Kundi la simba wakiwa wanakula nyama ni dogo tu. Kundi la wala mzoga ni utitiri.
Kwenye biashara, masoko yote ni pyramids. Wapo walaji walio juu ya food supply chain. Na wapo walio chini. At the bottom.
Kama unapata utitiri wa engagement kwenye post zako basi, kama tulivyoweka bayana hapo juu, umegusa kundi la wenye kipato kidogo. Yaani watu WOTE.
Maudhui yenye chembe za hisia, mihemko, mzaha na upuuzi wenye kuchekesha huvutia watu masikini. Kundi hili linapenda burudani kwasababu huwasahaulisha uhalisia wa hali zao ngumu.
Hapo sahau kuhusu kuwauzia bidhaa. Unaweza kuongelea matatizo yao na ukawagusa, lakini pesa yao inaenda kwenye mahitaji ya lazima.
Labda kama content yenyewe ndiyo bidhaa. Yaani unalipwa na YouTube kwa views za masikini hawa. Yule jamaa yetu kapotea njia maana LinkedIn hawalipi mtu. Bora angekuwa X kwa maokoto ya Elon Musk.
Maudhui ambaya ni ‘ngumu kumeza’ yaani high tech, high intelligence —haya huvutia kundi dogo tu la watu. Hapa hatupo tena chini ya pyramid. Hawa wanaweza kununua.
Ok, turudi mbugani; unakimbiza swala au utakula kilichosazwa?
0 Comments