Mwanachuo Lazima Ufanye Haya ili Ukwepe Kuwa Jobless Baadae

Written by Anthony Charles

Anthony Charles is a young web designer | Content writer. He build websites for business growth.

Posted June 17, 2023

Hakuna muda mzuri wa kukabiliana na unemployment kama muda ambao uko chuo.

Wengi huja kulifahamu hili tayari jua limeshazama, muda huo upo nyumbani, pengine hata kupata fedha ya kujikimu au ya vocha ni kipengele yaani kuipata ile buku mbili mpaka uende ukafanye kazi za vibarua ndio uipate.

Tafuta jambo lolote ufanye ukiwa chuo kama side hustle yako. Itakusaidia kupata uzoefu wa hapa na pale.

Kitu kizuri ni kwamba leo hii upo chuo, unapokea boom, tukiongelea suala la bando kwako saivi siyo shida basi tumia muda huo kufanya mambo ambayo baada ya kumaliza chuo usihangaike kutafuta kazi.

Haya ndiyo mambo sita ambayo Mwanachuo Lazima Ufanye Haya ili Ukwepe Kuwa Jobless Baadae

1. Jiunge na mitandao ya kijamii muhimu kama vile LinkedIn na Twitter

Ni imani yangu tayari una account ya Twitter, Instagram, Facebook lakini nina shaka kama App ya LinkedIn unayo.

Anyways, LinkedIn na Twitter ndiko maarifa yalipo, huko utakutana na waajiri mbalimbali (Recruiters/Employers). Watu kama hawa inawezekana usiwaone kipindi unaanza ila jinsi utakavyozidi kuonyesha uwepo wako kwenye majukwaa hayo, ndivyo utakavyojiweka katika nafasi nzuri ya kuonekana kuliko wale wanafunzi wenzako. 

Huko utapata kujifunza mambo kadha wa kadha yanavyoenenda kwenye tasnia yako, pia itakusaidia kuelewa mapema ni nini ufanye ili baadae usije kupishana na gari la mshahara. Huko kuna watu wenye digital skills za kutosha ukiwa tu unapitia tweets au posts zao kuna mengi utajifunza.

Itakusaidia kuelewa jinsi mambo yanavyofanyika kwenye industry unayosomea. Siyo unamaliza chuo, unaambiwa nafasi zipo na zinahitaji mtu anayejua vizuri Microsoft Access ndiyo ukute na wewe ulivipuuzia kipindi upo chuo.

Katika ulimwengu tuliopo simu au laptop yako ni siraha tosha inayoweza kubadilisha historia ya maisha yako, itategemea unaitumia kwa namna gani. Jambo la kufanya install app ya Twitter au LinkedIn na ujifunze jinsi ya kutengeneza Linkedin profile nzuri sasa hivi.

2. Follow watu wanaoshare madini

Utapata maarifa mengi kwa kufollow watu wanao-share madini acha kufollow follow watu watakaokutoa kwenye line yako kwa sababu mtu ukimfollow timeline yako itajaa posts zake zenye utopolo ndani yake.

Ubongo nao ulivyo wa ajabu utaanza kunasa na kuweka kumbu kumbu juu ya yale uliyoyaona. Medulla Oblangata itayahifadhi taarifa hizo, hatimaye na wewe unakuwa mtu wa hovyo vile vile.

Usiingie kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuangalia udaku na kuscroll scroll kusiko na maana bali ingia na akili ya kujifunza au akili ya kibiashara. Mitandao ipo ili uitumie ikuletee faida siyo ikutumie ikuletee hasara.

Ukikutana na post ambayo haijakupendeza. Fanya hivi:

  • Unfollow kama umemfollow
  • Mmute
  • Block huyo mtu
  • Hit not interested in this post

Hivi ndivyo utaweza kuchuja maudhui yapi uyaone na yapi usiyaone. Mtandaoni kuna kila aina ya watu na kila mmoja ana malengo yake usipotezwe kwenye malengo yao.

3. Ongeza maarifa kupitia Online Courses

Internet imerahisisha maisha, leo hii unaweza kusoma popote ulipo na cheti ukitaka unapewa. Ulimwengu tulio nao bila kunoa ujuzi wako utajikuta unapitwa na wakati kila siku.

Jifunze maarifa mapya kila siku, watu wanaoweza kujitofautisha na kupata fursa kidigitali ni wale waliowekeza nguvu zako katika kujifunza maarifa mapya ama kujiendeleza katika career zao. Huwezi kuwa vizuri ikiwa huna utaratibu wa kunoa ujuzi wako kila siku.

Vijana wengi chuoni hawanaga muda kabisa wa kuchukua course mtandaoni kujifunza maarifa mbali mbali basi wewe jitahidi kuwa mtu wa tofauti chukua hizo courses nakwambiaje lazima tu utawazidi kwa kiasi chake halafu zisake fursa zinazoendana na maarifa uliyoyasoma.

Course yoyote unayoitaka inapatikana mtandaoni ni suala la kuchukua simu na kuingia YouTube, andika course unayotaka usome mfano, Project Management full course, kwa click moja unamaliza course ukiwa na maarifa ya kutosha.

LinkedIn Learning pia inatoa courses mbali mbali kwa mwezi mmoja baada ya kujiunga LinkedIn premium Bure kabisa.

Pia kuna majukwaa mengi ambayo unaweza kuchukua course unayoitaka kama vile Linkedin learning, simplilearn, Udemy, Coursera, Class Central n.k huku unafundishwa real life experience tofauti na mwalimu darasani anaekufundisha ili amalize syllabus.

4. Kuwa vizuri kwenye lugha (written and spoken)

Asilimia 90% ya mazungumzo mtandaoni hufanyika kwa njia ya maandishi, hivyo ni vizuri ukajinoa zaidi katika kuandika na kuwasilisha maudhui/ujuzi wako kwa watu.

Njia nzuri ya kujinoa ni kuanza leo kwa kuandika mawazo uliyonayo kichwani kwenye notebook au applikesheni yoyote ikiwezekana uwe unapost huko mtandaoni hata kama kiingereza au kiswahili kimekaa upande. Post leo, kosea jifunze tena mdogo mdogo mwisho wa siku unakuwa vizuri.  

Ukiwa chuoni jitahidi kupost kila siku au mara mbili kwa wiki ikiwa vipindi vimebanana sana. Ule muda unamaliza chuo, utakuwa na kundi kubwa la watu wanaokuhitaji ufanye nao kazi au uwafanyie baadhi ya kazi zao.

Mitandao huwa haina maana saana kwa macho ya mwanafunzi lakini subiri umalize ndio utajua umuhimu wake. Haijalishi unasomea nini kuwa na digital presence ni lazima, unaona akina Mo Dewj wako kule unafikiri masihara!

Muhimu: Post vitu vya msingi ambavyo mtu akisoma aseme kweli huyu kijana au huyu dada anajua.

5. Anza kufanya kazi ukiwa bado upo chuo (freelancing au virtual internship)

Tafuta kazi ambazo unaweza kufanya ingali bado unasoma, ukiwa chuo ndio muda wa kujitolea kwenye taasisi, kampuni mbalimbali. Fanya kazi as a freelancer kwenye majukwaa mbalimbali kama vile Upwork, Freelancer, Fiverr, Remototask.

Muda mwingine vitu unavyofundishwa darasani nitofauti kabisa na vile vinavyofanyika kwenye industry, hivyo ni bora kuyajua haya mapema na kuyafanyia kazi ili pindi utakapomaliza chuo isiwe changamoto kwako. 

Usisubiri mpaka umalize chuo ndio uanze kuomba kazi, najua unajua kule nyumbani hali ilivyo yaani kupata kazi ni mtiti, ukimaliza chuo ukaenda nyumbani, ndiyo imeisha hiyo.

6. Kuwa mtu mwenye haiba (personality) ili umma wa digitali uvutiwe na wewe

Kila siku jitahidi kuwa mtu wa tofauti na wengine, fanya vitu ambavyo watu wengi hawavifanyi ilimradi unaviamini, ni halali, utaonekana kuwa ni mtu wa pekee, na kwa upekee huo utajinyakulia fursa kedekede.

Kuwa mtu wa kujifunza kila kukicha kwa kusoma vitabu, articles, hudhuria mikutano, seminar au online events. 

Tatizo la ajira halitakaa liishe bali litaongezeka maradufu. Juhudi zako tu ndizo zitakazokuokoa.

Hakuna chuo kinachoweza kukufanya ukwepe kuwa jobless baadae, zaidi ya kuweka juhudi zako binafsi katika kuitengeneza kesho yako. Hatima ya maisha yako ipo mikononi mwako.

0 Comments

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Governments vs Social Media: Build That Website

Governments vs Social Media: Build That Website

It is not a wise idea to put all your eggs in one basket. Especially if you have little ownership of that basket. Recent feuds between governments and social media giants highlight the risks of relying on third-party platforms for business. Here’s why owning your...

Introducing Tanzlite Host: The New Web Hosting Player in Tanzania

Introducing Tanzlite Host: The New Web Hosting Player in Tanzania

Earlier this year, we introduced Tanzlite Host. This is not just another name in Tanzania's web hosting services; we're rewriting the rules. Here's how our unique approach to business is setting us apart and why it's the most profitable model in the industry: A...

Products From Tanzlite