Linkedin ni mtandao wa kidigitali ambao unaunganisha watu wa kila aina kutoka pande zote za dunia hasa vijana wanaotafuta kazi, wajasiriamali wanaotaka kukuza biashara zao, kuboresha kazi zao na makampuni yanayotafuta wafanyakazi nayo pia yapo Linkedin.
Unaweza kuchukulia masihara ila wataalamu wengi wako kule yakiwemo makampuni, kule watu waliotengeneza jina wanaingiza pesa bila hata kwenda ofisini kuomba kazi, wengi wanafanya kazi kama freelancer.
Jinsi ya kujiunga linkedin
Kuna namna mbili za kujiunga linkedin, namna ya kwanza ni kusanikisha/kuinstall linkedin app kupitia playstore. Andika Linkedin app kwenye search bar bonyeza iyo application ya blue kisha install. Baada ya kuinstall endelea na usajili, Linkedin app itaonekana kama hapo chini.
Namna nyingine ni kujisajili kupitia website ya linkedin, bonyeza Linkedin signup jaza taaarifa zinazohitajika, kuwa na kumbukumbu juu ya taarifa unazoziweka ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza baadae kama utasahau neon siri.
Sasa tumeweza kujiunga na kusign in, Linkedin watakutumia ujumbe kwenye email yako ili kuthibitisha kama gmail yako iko active, kinachofuata ni kumalizia usajili kwa kujaza taarifa zako ipasavyo kwani hizo taarifa ndizo zitakazokaa kwenye profile yako ya Linkedin
Tayari Tumeshatengeneza Akaunti, Sasa Twende Tukaifanye Profile Yako Iwe ya Kitaalamu.
Awali ya yote Linkedin siyo facebook, huku kidogo inabidi ujiweke katika mazingira mazuri uonekana as a professional, huku ndiko wateja wako walipo na ndiko utakapopata fursa mbalimbali za kukutana na watu, kushare idea, kubadilishana mawazo na watu mbalimbali kulingana na tasnia uliyopo.
Bila kupoteza wakati haya ni mambo muhimu inabidi uyafanye ili kuboresha profile yako.
1.Profile picture.
Hakikisha picha unayoweka kwenye profile inakutambulisha kama mtaalamu kwenye tasnia yako. siyo unapiga selfie ndio unatuwekea kwenye profile, Recruiters, wateja watakuona hauko serious. Picha hiyo iwe karibu na kamera, ionekane vizuri. Picha yako ndiyo utambulisho wako.
2. Banner.
Hapa utaweka background picture, texts au quote inayoendana na fani yako. Size ya background image huwa ni 1128 x 191. Wengine pia huweka namba zao za simu na email. Ni vizuri ukachagua kipi kinafaa uweke kuliko kuacha blank. Angalia mfano hapa chini.
3. Kichwa cha profile yako.
Hapa nazungumzia jina lako kamili na headline title ambayo itaonekana mwanzoni kabisa mwa profile yako. Hakikisha headline inajibu wewe ni nani, unasaidia nini?
Kufanikisha hili angalia hapo juu kushoto kuna kitufe kama kalamu bonyeza hicho na jaza taarifa zinazohitajika. Mfano Headline* yangu ni Built my brand while in college from 500+ to 7k people. Helping you do the same. Web developer & designer | Content Writer.
4. Kazi na Elimu.
Ili kuifanya profile yako inawili vizuri, hapo hapo kwenye profile kuna sehemu imeandikwa Open to work bonyeza hicho kipenseli, halafu weka cheo cha kazi unayofanya (job title) n.k
Ukishafika kwenye visibility ruhusu recruiters only, hiyo nyingine siyo nzuri kuitumia kama kweli wewe unataka uonekane mtaalamu katika tasnia yako.
5. Experience/uzoefu
Pia utashuka chini kwenye Experience, hapo utaweka shule, makampuni au taasisi ambazo umeshawahi kufanyanayo kazi. Elezea kwa kiasi gani umeshiriki katika kuongeza ujuzi wako, vitu gani ulifanya n.k.
6. About
Hapa inatakiwa uelezee fani yako japo kwa kifupi, weka bayana nafasi uliyopo kwa sasa, unafanya nini, unatatua changamoto zipi, kwa namna gani, uzoefu wako ni upi kisha unaweka vitu ambavyo unaweza kuwasaidia watu wengine. Angalau ianzie aya mbili.
7. Mpangilio/Setting.
Mkono wa kulia juu kwenye profile yako kuna ikoni ya setting, ibonyeze shuka chini kidogo showing profile photo ruhusu kwa linkedin members wote.
8. Usisahau kuwasha creator mode.
Hapa utaweka vitu utakavyokuwa unaongelea katika machapisho yako ya kila siku. Kwa kufanya hivi naamini kwa asilimia 90 profile yako itaonekana bora na ya kiprofessional zaidi.
Tumalizie, Linkedin pia inatoa fursa ya kujifunza course mbalimbali bure ndani ya mwezi mmoja. Je unapataje ofa hii?
Ni rahisi tu, pale unapoingia linkedin home page kwa juu mkono wa kushoto kunaonekana profile picture yako, ibonyeze halafu angalia chini wameandika activate premium, pabonyeze halafu endelea na maelekezo.
Baada ya hapo unaweza kujiunga linkedin learning ukapiga course mbali mbali ukishamaliza unapewa na cheti kabisa, ni wewe tu kufanya maamuzi leo.
Muhimu: Kuwa makini kwenye Akaunti utakayotumia kwenye premium kama unaona siyo vizuri kutumia kadi yako ya bank unaweza kutengeneza M-Pesa VISA Card bure ndani ya dakika moja.
Baada ya kufanya hivyo inabaki kazi ya kujimwanga kwenye jukwaa kuwakilisha kile ulicho nacho hapa naongelea kupost, kushiriki kwenye mazungumzo na jumuiya ya Linkedin, kuendelea kuwa hai.
Thanks for good explanation i believe this will help me to create quality account profile soon other possible. Be blessed.