Siri Ya Mafanikio Mtandaoni, Nunua Kitabu Hiki

Written by Shukuru Amos

I am the founder of Tanzlite Digital, Creator, Author of Mbele Ya Muda, and the most followed Tanzanian marketer on LinkedIn.

Posted November 20, 2023

Naitwa Shukuru Amos. Kabla sijakudokezea siri ya mafanikio mtandaoni, naomba nikupe stori yangu fupi: Hapo Mwanzo hapakuwa na jina Shukuru Amos kwenye uso wa dunia ya digital marketing. Yote yalianza mara baada ya mimi kutangaziwa kwamba nina wiki mbili zimebaki nifanye mtihani wa mwisho chuoni.

Hapo ndipo nikagundua ninaelekea mtaani nikiwa jobless and unemployed. “Nikimaliza chuo nitafanya nini?” nilijiuliza.

Nikisema nirudi kwetu kijijini, hakukuwa na ishu ya kufanya. Nikisema nibaki ndani ya jiji la Dar es Salaam, hapa pia hakukuwa na ishu ya kufanya.

Je, nilimua lipi? Nilianzaje? Nimejifunza yapi ndani ya miaka mitano kufikia hatua ya kazi kunifatuta mimi na si mimi kutafuta kazi? Yote haya nimeeleza ndani ya kitabu changu kiitwacho; MBELE YA MUDA: Kama Unataka Mali, Utaipata Shambani.

Tunakoelekea, kila mtu atalazimika kuingia kwenye uchumi wa digitali. Ndipo kutakuwapo kilio na kusaga meno kama hujajiandaa.

Shukuru Amos

Tatizo la Vijana wengi Tanzania ukiwemo wewe

Vijana wengi wana shida ya kujiwasilisha kizembe kwenye maombi ya kazi. Tatizo hili linajidhihirisha pia wanapoingia kwenye soko la uchumi wa digitali.

Haiwezekani mtu una followers 10,000 halafu bado unalalamika kuhusu kukosa kazi. Haiwezekani! Lakini ndiyo shida waliyonayo Freelancers wa Kitanzania. Wengi hawana jina lenye hadhi.

Pamoja na ukweli kwamba uchumi wa digitali unaweza kutufanya kuondokana na ukosefu wa ajira na umasikini, inasikitisha kwamba vijana wengi hawajawahi kupata pesa mtandaoni.

Kama unachangamoto hii, una matatizo manne. Nitakupa mawili hapa (mengine ndani ya kitabu):

  1. Unashindwa kuandika kwa sauti yenye mamlaka.
  2. Unashindwa kuonyesha ukomavu wa fikra kupitia maandishi.

Hapo zamani za kale, walikuwepo watu wanaitwa Alchemists. Hawa walikuwa wanajaribu kubadili madini ya risasi kuwa dhahabu. Lakini mwishowe walikata tamaa. It was impossible turning lead into gold. Mimi sitaki wewe ukate tamaa.

Unaweza kubadili content kuwa jina lenye hadhi na kufanya fursa zikutafute. Siyo wewe kuhangaika kutafuta fursa muda wote.Kufahamu tatizo la 3 na la 4, pamoja nini cha kufanya —nunua kitabu changu.

Maoni ya baadhi ya waliosoma kitabu hiki

Je, Mitandao inalipa au hailipi?

Hebu Fikiria Upo Kwenye Stage Hii:Huna wasiwasi juu ya wapi na namna gani utapata mteja, au ajira. Unapata meseji (qualified leads) 4-9 kwa wiki za watu ambao wako interested kufanya kazi nawewe.

Uko vizuri kwenye kushawishi mkikutana au kwenye simu. Watu ni wengi kuliko unavyoweza ku-handle. Huna tena habari za kuandaa CV, kujitolea au kwenda kuongeza mastaz. Unafanya kazi ukiwa nyumbani au popote. Foleni za Jiji tena basii.

Hayo yote yanawezekana. Mimi mwandishi wa kitabu hiki nipo kwenye stage hii sasa. Sitafuti kazi. Kazi zinanitafuta! Kama mimi kijana kutoka uskumani ndani ndani nimeweza, hata wewe unaweza. Mitandao inalipa ndugu yangu!

Umechoka kuandika Dear Sir/Madam bila kupata majibu?

Kama kutuma maombi ya kazi umeshatuma sana. Vyeti unavyo vya kutosha. Pengine umejaribu mitandao lakini unaona kama wembe ni ule ule. No job!

Ndani ya MbeleYaMuda, nimeandika “Usiwe mtafuta kazi maarufu” kwani hakuna mtu anasema “Muone fulani huwa anatafuta kazi”. Watu husema “Muone fulani huwa anafanya hicho kitu.”

Mbele Ya Muda ni kitabu chenye MADINI yatakuyokufanya ujione ULICHELEWA kuanza kufaidika na NGUVU ya Mtandao.

Kimeandikwa na mimi, the most followed Tanzanian marketer on LinkedIn. Ambaye uandishi na uwasilishaji wangu unafuatiliwa sana kwenye mtandao huo.

Moja kati ya mada zilizomo ndani ya MbeleYaMuda, utajifunza Personal Branding, Uandishi na Uwasilishaji unaoleta Pesa na KUHESHIMISHA Jina. Pia utajifunza kuhusu Biashara Mtandaoni, Saikolojia ya Maudhui na mengine tufanye siri yako. Maana yana ukakasi kidogo kuyasema hadharani. Lakini ndiyo siri ya mafanikio mtandaoni.

Majibu, Maujuzi na Maujanja YOTE Utayapata ndani ya kitabu hiki.

Kitabu hiki kwasasa kinapatikana kwa mfumo wa soft copy pekee. Bei ni Tsh 29,900/=

BOFYA HAPA kununua kitabu, au BOFYA HAPA kunicheki WhatsApp. Au nipigie 0742 085 089.

0 Comments

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Governments vs Social Media: Build That Website

Governments vs Social Media: Build That Website

It is not a wise idea to put all your eggs in one basket. Especially if you have little ownership of that basket. Recent feuds between governments and social media giants highlight the risks of relying on third-party platforms for business. Here’s why owning your...

Introducing Tanzlite Host: The New Web Hosting Player in Tanzania

Introducing Tanzlite Host: The New Web Hosting Player in Tanzania

Earlier this year, we introduced Tanzlite Host. This is not just another name in Tanzania's web hosting services; we're rewriting the rules. Here's how our unique approach to business is setting us apart and why it's the most profitable model in the industry: A...

Products From Tanzlite