Jinsi ya Kupata Wateja Mtandaoni Kupitia Matangazo Mguso (PPC Advertising)

image showing google search results page with PPC results

Written by Shukuru Amos

I am the founder of Tanzlite Digital, Creator, Author of Mbele Ya Muda, and the most followed Tanzanian marketer on LinkedIn.

Posted July 26, 2020

Kukua kwa matumizi ya internet nchini Tanzania kumerahisha uwezekano kukuza biashara yako na kufikia wateja wengi mtandaoni. Zipo njia nyingi za kuweka biashara yako kwenye mtandao ikiwemo tovuti, mitandao ya kijamii, kupitia WhatsApp, email na nyingine nyingi.

Katika zama hizi za digitali, watu hufanya utafiti wa bidhaa wanayotaka kununua kabla ya kufanya maamuzi ya kununua. Utafiti wao mwingi unahusisha kutafuta (Search – au kugugo) kwenye injini za utafutaji pamoja na kusikiliza ushauri wa watu ambao wamewahi kutumia bidhaa hiyo.

Kwa wenye biashara zenye website, ipo njia ya kunasa wateja kwa haraka. Njia hii ni kutumia matangazo mguso (PPC ads). Njia hii huitaji kusubiri miezi kadhaa kuanza kupata watembeleaji kwenye tovuti yako kama ilivyo  kwenye mpango wa SEO.

Ukiwa mfanyabiashara, kuonekana kwenye matokeo ya utafutaji (search results) ni fursa kubwa ya kutangaza bidhaa au biashara yako ili watumiaji hawa wa mtandao (internet) waweze kuona biashara yako. 

Maana yake kama hauko online, watafutaji hawa watakukosa na mshindani wako aliyeko online atapata fursa ya kunasa hawa wateja.

 

Injini za utafutaji kama vile Bing, Google na Yahoo zina huduma ya kuweka matangazo kwenye matokeo ya utafutaji (search results) 

Kitaalamu inaitwa Paid Per Click Advertising (PPC). Ni aina ya kutangaza bidhaa au huduma kwa kununua maneno maalum (keywords) yanayohusu biasha yako ambapo utaweza kuonekana endapo mtumiaji akitafuta kwa kutumia maneno hayo. Maana ya jina Pay Per Click ni kwamba unalipa endapo mtu atabofya tangazo lako na kuzuru tovuti yako.

Matangazo haya hukaa mwanzoni mwa ukurasa wa matokeo ya utafutaji (search engine result page), yakifuatiwa na matokeo ya kawaida (organic results). Pia yanaweza kuonekana sehemu nyingine ndani ya results page.

Tazama picha ifuatayo:

Ufafanuzi kuhusu picha ya juu.

  1. Ni uwanja wa kutafutia (search bar) ambapo mtu ametafuta ‘stuffed animals’
  2. Vertical navigation (hapa unachagua uone matokeo ya Picha, Bidhaa, Video, Maeneo au Habari)
  3. Taarifa kuhusu matokea ya utafutaji (search results information)
  4. Haya ndiyo matangazo mguso (PPC Ads) 

PPC Inafanyaje Kazi? 

Matangazo haya hutolewa kwa ushindani au mnada. Wenye biashara hushindania maneno kwa kuweka dau kubwa juu ya mwenzake ili apate kuonekana  endapo mtu ‘atagugo’  kwa kutumia maneno hayo. 

Hivyo, mambo mawili ni muhimu kuzingatiwa;

  1. Dau lako kulinganisha na dau la mwenzako (auction) 
  2. Ubora na uhalisia wa huduma yako (quality and relevance) 

Hebu tuangalie mfano ili upate kufahamu zaidi:

Tuseme unamiliki hoteli na unataka kutangaza kupitia matangazo mguso. Washindani wako wengine kama kampuni mbili hivi  nazo  zinataka kutangaza. Hapo 

  • Best hotels in Serengeti
  • Serengeti National Park 
  • Tanzania adventures 
  • Best hotels in Tanzania
  • Luxury resorts in Tanzania

Tuseme wote mmechagua maneno hayo juu. Wewe ukaweka dola mbili per click, mshindani wako akaweka dola nne kwa kila mtu atakapo bofya tangazo. Hapa maana yake mwenzako atakuwa anaonekana zaidi kuliko wewe kwenye paid search results

Mara nyingi gharama za malipo per click hupanda kutegemea na ushindani na eneo unalotaka kutangaza. Kwa mfano, wewe ni Hosting company au Insurance company katika jiji la New York, hapo ushindani kwenye keywords utakuwa mkubwa hivyo utalazimika kuweka pesa nyingi.

Lakini kwa nchi kama Tanzania, makampuni mengi hawatumii PPC advertising, hivyo linaweza kuwa chimbo zuri kwako wewe kunasa wateja. Unaweza kujikuta ni wewe tu unayetangaza katika sekta yako.

Lakini pia kuna vigezo vya ubora na uhalisia wa maudhui na jinsi tovuti yako ilivyoundwa. Hivi vinaweza kuathiri uwezekano wa kuonekana kwenye matokeo ya utafutaji. Ikumbukwe lengo la google ni kutoa matokeo sahihi kwa watumiaji wake na kuhakikish user experience ni ya kuridhisha. Hivyo unaweza kuwa na dau dogo kuliko mwenzako lakini bado ukaoneka.

Vipi kuhusu ufanisi wake? 

Ufanisi wa aina hii ya matangazo ni bora zaidi kwasababu hapa unatangaza kwa watu ambao tayari wako interested na biashara yako. Yaani unalenga wateja ambao tayari wanatafuta huduma yako (customers who are actively searching for your product or service). 

Kupata umaarufu (awareness and recogntion) wa biashara yako mtandaoni inachukua muda kutegemea na maarifa na jitihada ulizo wekeza. Lakini kwa kutumia matangazo mguso (PPC) unaweza ukajulikana na kuanza kuvutia wateja kwa muda mfupi sana. Ni jambo la siku au masaa tu. 

Unahitaji kufahamu zaidi au kufanyiwa huduma hii kwenye biashara yako? Wasiliana nasi HAPA

3 Comments

  1. Linah

    Nafanya biasharaa ya nguo online napat shdaa san upand wa watej

    Reply

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Governments vs Social Media: Build That Website

Governments vs Social Media: Build That Website

It is not a wise idea to put all your eggs in one basket. Especially if you have little ownership of that basket. Recent feuds between governments and social media giants highlight the risks of relying on third-party platforms for business. Here’s why owning your...

Introducing Tanzlite Host: The New Web Hosting Player in Tanzania

Introducing Tanzlite Host: The New Web Hosting Player in Tanzania

Earlier this year, we introduced Tanzlite Host. This is not just another name in Tanzania's web hosting services; we're rewriting the rules. Here's how our unique approach to business is setting us apart and why it's the most profitable model in the industry: A...

Products From Tanzlite