Kwanini Unafeli Mtandaoni

Kwanini Unafeli Mtandaoni

Hebu tuwe wakweli Kuhusu Kupata Wateja Mtandaoni . Tangu uamue kuuza maarifa mtandaoni hakuna kilichotokea. Juhudi za kupost na kucomment kila mara zinaishia kuwa mbuzi wa masikini –hazizai matunda. Watu hawakufuati kutaka huduma yako.

DM yako ni kavu kama jangwa la Kalahari. Hadhira uliyonayo (followers) hawakufuatilii. Likes na comments ni za kumulika kwa tochi. Hata Likes zikiwa nyingi, bado mauzo ni sifuri.

Mbaya zaidi, hata haujui kwanini unafeli mtandaoni. Haujui shida iko wapi!

Ukweli ni kwamba huna hadhira inayokuchukulia serious. You don’t have an audience.

Jina lako mtandaoni halina hadhi, hujaweza kujitofautisha na ndiyo maana watu hawaoni sababu kwanini wakuchague wewe. You are just another voice in the noise.

Hii makala itakusaidia sana.

Nimeamua kuandika kitu ambacho utakifanyia kazi papo na kuanza kona mabadiliko.

Twende kazi!

Shida ya kwanza: Huna kitu kinaitwa “narrative”

Kosa kubwa unaloweza kulifanya mtandaoni ni kuingia bila kuwa na simulizi inayokutambulisha. Hapa siongelei historia ya maisha yako sijui wewe ni nani, ulizaliwa wapi ikaja ikaenda….hapana. Hiyo ni sehemu tu ya kuunda narrative.

Kuwa na narrative maana yake ni ule mjumuiko wa stori, mawazo na vitendo vinavyojenga taswira yako ya kipekee. Mambo gani unasimamia, yapi unayapinga —yaani how are your choices, values and action build up a narrative around your identity?

Unataka mfano? Sawa.

Tuseme haupendi kuajairiwa, ulijaribu ukaacha kazi na sasa uko na mishe zako binafsi (Solopreneurship).Kwahiyo narrative yako itakuonyesha kama mtu anayependa uhuru na ni mjasiriamali. 

Mfano mwingine wa kuunda narrative yako ni kuunda misemo yako na namna pekee ya uwasilishaji. Yaani hautumii maneno na lugha iliyozoeleka kwenye niche yako.

Hakikisha una “kaongelee” kako, misemo yako, misimamo na mitindo yako.

Hakikisha una kaongelee kako, misemo yako, misimamo na mitindo yako.

Shukuru Amos

Kwa mfano mimi; nina misemo na misimamo yangu maarufu kule LinkedIn:

  • “Kataa Fikra Elekezi”
  • “Social Rhetoric”
  • “Content Alchemist”
  • “Holiday posts are useless”
  • “Awards are useless” 

Usitumie msamiati wao. You’re not just another corporate person using corporate verbatim.

Kama kila mtu kwenye B2B anasema yeye ni “Best au award winning service provider” basi kaa mbali na utambulisho wa namna hiyo. Toka kivingine. Utofauti unakumbukwa. Utofauti unakaa akilini.

Shida ya pili: Una Uoga na Aibu

Tatizo lingine linalopelekea kufeli mtandaoni ni kwamba huna ujasiri wa kuongea kwa sauti yenye mamlaka. You’re being too safe. And shy.

Acha kuremba maneno unapoongelea upuuzi unaofanyika in your niche. Even worse, umeingia kwenye niche fulani na ukafanana na wote walio kwenye hiyo niche. 

Sasa nani akusikilize ikiwa umeingia na kuwa kama uliowakuta?

Be a contrarian. Kosoa kile ambacho wengi wanakiamini kwa kuonyesha ama kiko overrated au ni simply useless. Kataa Fikra Elekezi zilizomo kwenye tasnia hiyo.

Hivyo ndiyo utaweza kuonekana na kuchukuliwa serious.

Shida ya tatu: watu hawajali

Umeingia mtandaoni ukijua unachokijua. Lakini hujakaa kudadavu ni kina nani hasa unawalenga. Wanahitaji nini? Kipi kinawakosesha usingizi?

Usiwe tu na hadhira ya jumla, ni lazima uchimbe mpaka umpate unayemtaka.

Kama uko kwenye fitness, unaweza kuamua unataka kuhudumia wanaume au wanawake? Pengine ukaenda niche zaidi ukasema fitness coach for stay home moms, au fitness coach for busy female corporate workers.

Shida ya nne: Maudhui yako yanaboa

Hii ni changamoto ya uwasilishaji. Uandishi wako hauna ladha, hauna vichombezo shirikishi kama vile misemo na tamathalli semi. Yaani unawasilisha tu ilimradi.

Kama ni video basi usemaji, mazingira na vielelezo vya mwili havivutii.

Shida ya 5: Hauko serious

Hapa kuna mambo mawili; bidii na kujigharamia kuwa bora. 

Nikuulize swali, ndani ya miezi 9 iliyopita umewahi kulipia maarifa? Yaani kununua kitabu, course, coaching session. Au paid subscription kama vile Medium Membership, X Pro, newspaper subscription n.k. Kama jibu ni hapana au haukumbuki basi hauko serious.

Kuhusu bidii: Kama mwezi huu unajaribu, mwezi ujao hatukuoni; halafu baada ya muda unakuja tena unafanya fanya unapotea tena. Hapa si bora utafute ajira na ukawe mfanyakazi mtiifu. Mafanikio mtandaoni yanahitaji watu wanaojituma.

Kama haujui kinachokufanya usifanikiwe mtandaoni, hauwezi kupata suluhu. Kama haujui ni aina gani ya maudhui yanafanya vizuri, utaendelea kubahatisha.

Nina matumanini makala hili imekufanya uhoji mkakati wako mzima wa kuuza maarifa mtandaoni.

Ninaitwa Shukuru Amos. Ni mwandinshi wa kitabu cha Mbele Ya Muda. Ndani ya hiki utajifunza kuhusu personal branding, maudhui na biashara mtandaoni. Pia nimeandika Mwongozo mfupi kukusaidia Kutengeza Profile Yako ya LinkedIn au X mwanzo mwisho. 

Mwisho

Unaishi kwenye Ulimwengu wa Digitali. LAKINI kwanini habari za kupata PESA na MAFANIKIO Mtandaoni unazisikia kwa watu wengine tu? Na ukiangalia bado KIJANA kabisa. Ni kweli umekubali kuwa mtazamaji kwenye Uchumi wa DIGITALI? Hapana bwana!

Jipatie Pesa Kwa Kuandika Kwenye Jukwaa La Medium

Jipatie Pesa Kwa Kuandika Kwenye Jukwaa La Medium

Habari kwa Digital Writers Tanzania. Sasa Unaweza kujipatia pesa kwa kuandika kwenye jukwaa la Medium. “We’ve added 77 countries to the Medium Partner Programtaarifa rasmi kutoka Medium ilisema mnamo August 6, 2024. 

Kabla ya hapo, Tanzania haikuwemo miongoni mwa nchi ambazo writers waliweza kujipatia pesa kupitia makala zao kusomwa. In fact, hakukuwa na nchi hata moja ya Afrika.

Kama ilivyo kwa majukwaa mengine yanayolipa watengeneza maudhi, kuchelewa kwa Tanzania kuwa kwenye orodha ya Medium Parter Program ilitokana na shida ya njia ya malipo. Wanatumia Stripe kugawa malipo. 

Mwezi Februari nilijaribu kujiunga nikaambiwa “You are located in a country that is not eligible for payouts.” Basi kwenye orodha hii mpya, Tanzania imo. Kazi kwako msaka maokoto mtandaoni.

Je Jukwaa la Medium ni Nini?

Mtandao wa Medium ni kama YouTube lakini kwa waandishi. Ni jukwaa la waandishi wa makala zinazohusu mada mbalimbali. Yaani unaweza kuandika chochote kwa ujuzi, uzoefu au maoni yako. Medium inakuwezesha kumiliki blog yako ambayo tayari ina wasomaji maana watumiaji wa jukwaa lile ni takribani milioni 100 kila mwezi.

Je Unalipwaje kwa Kandika Medium?

Kupitia Medium Partner Program, ukiandika makala yako ikapata engagement kama vile likes/claps, comments na activity zingine kama highlights, unaweza kujipatia kiasi fulani cha pesa (in dollars). Zikifika dollar 10, zitatumwa kwenye akaunti yako ya benki yoyote hapa Tanzania.

Masharti ya Kujiunga.

Ni lazima uwe mtumiaji wa Medium Pro, wenyewe wanaita kuwa Medium Member. Ni dola $5 kwa mwezi.  Kama hauko tayari kutumia pesa ili upate pesa basi fursa hii si yako. Pia uwe umechapisha makala kwenye jukwaa hilo kwa kipindi cha ndani ya miezi 6 iliyopita. Hii maana yake: Unaweza kujiunga leo na ukaandika makala zako mbili au tatu hala ukaomba kujiunga kwenye programu ya kulipwa. Epuka kutumia AI kuandika makala zako, hiyo hawataki kabisa. Wanataka ubora na uhalisia.

Zaidi ya hapo hakuna masharti magumu. Unaweza soma zaidi hapa kufahamu Medium Partner Programu ni nini.

Je ni Nini cha Kuandika?

Andika chochote unachokijua, uzoefu wa maisha au ujuzi wako kitaaluma. Hakuna masharti ya nini cha kuandika. Ila ushauri tu kwako Mtanzania, andika kwa Kiingereza ili usijifunge kuandikia Waswahili tu.

Mimi binafsi ninaandika makala kwenye jukwaa la Medium. Unaweza kuni-Follow hapa.

Kutaka Kuuza Leo Leo Kunagharimu Biashara Yako

Kutaka Kuuza Leo Leo Kunagharimu Biashara Yako

Takribani wiki mbili zilizopita nilipigiwa simu na mfanya biashara mmoja akisema nimsaidie kutengeneza website ambayo itampatia wateja pindi watakapotembelea website yake anasema yeye yuko tayari kulipa kiasi cha pesa ilimradi tu hayo matokeo anayoyataka ayaone. 

Nilijaribu kumwelekeza kuwa kwa upande wa website sisi tutafanya mikakati ya SEO kuifanya website yako ipande kwenye search engine ili mtu anapotafuta huduma unayoitoa aweze kukuona kirahisi kwenye search result ya google. Tutatoa mapendekezo maudhui yaweje kwenye website ili kuvutia zaidi. 

Baada ya hapo mtu hawezi kushawishika kununua huduma yako kwa kutembelea website yako tu kuna mambo mengi ambayo humfanya mteja afikie maamuzi ya kununua huduma yako ikiwemo maudhui yaliyopo kwenye website, muonekano wake lakini pia utofauti wako kwa social media (positioning). 

Sababu kwenye website kuna sehemu ambayo huwa tunaweka social media links mtembeleaji aki-click hizo link je huko kwenye social media atakuona kama ulivyojionyesha kwenye website? 

Je, marketing strategies zako zitamfanya mtu arudi tena kwenye website au ashawishike kununua bidhaa yako, brand yako ikoje? 

Website pekee haiwezi kukufanya upate wateja mtandaoni bali itakujengea visibility shikamavu mtandaoni.

Gharama ya kutaka kuuza leo leo

Mfanya biashara anakupatia fedha kwa mashart kweli kweli: “Nataka ndani ya mwezi huu nianze kuona matokeo, nipate wateja wa kutosha, followers wengi, I want to see big numbers n.k.” 

Ni kweli hakuna mtu ambaye anataka kutoa pesa yake halafu baadae asione matokeo. Hakuna. Kila mtu anataka kuona amepiga hatua kwenye kazi yake lakini ni vyema kujua ukweli kuhusu kupata wateja mtandaoni kabla hujaazimia kuanza kuuza bidhaa/huduma zako mtandaoni.

Hivyo inabidi ujue kuwa kuna mchakato hapa katikati mpaka kuwapata wanunuzi wa bidhaa yako ambao ni :

  1. Brand awareness (Watu wakufahamu)
  2. Build community (Watu wakuamini)
  3. Conversion (Watu wahamasike kununua)

Wengi wanakosea hapa:

Anarusha matangazo kwa media either yeye mwenyewe au marketers aliowalipa, akitarajia kupokea utitiri wa wateja. Lakini, asilimia 80 ya simu zinazopigwa zinaishia kwa watu kuuliza maswali kisha wanachikichia mitini. Kweli, idadi ya followers inaongezeka, lakini cha ajabu, mauzo hayaongezeki. 

Kwenye tangazo, comments zinasoma 500k hadi 800k, lakini matokeo anayoyatarajia yanagonga mwamba kila kukicha. Mteja anaanza kuwalaumu marketers kwa kushindwa kufikia matarajio yake.

Ikiwa anapata yote hayo, shida ni nini hasa?

Shida kubwa ni kwamba mfanya biashara anataka kuuza leo leo kupitia tangazo au matangazo mawili matatu aliyoyatengeneza jambo ambalo ni gumu kulifanikisha, hajui umuhimu na kujenga msingi thabiti kwenye mitandao ya kijami ili apate matokeo anayoyahitaji. 

Kuanza na malengo ya haraka bila kuwekeza katika brand awareness na kujenga community ni sawa na kujenga nyumba bila msingi imara. 

Watu wengi wanaweza kuona bidhaa yako, lakini kama hawakufahamu au hawana imani na brand yako, hawatachukua hatua ya kununua.

Matokeo hayo yanatokana na ukosefu wa uelewa kuhusu safari ya mteja (customer journey) na jinsi inavyohusiana na mauzo. 

Kwanza, ni muhimu kuhakikisha kuwa watu wanakufahamu (awareness), kisha wanakutambua na kukuamini (community building), na mwishowe wanakuwa tayari kununua (conversion). Hii ni safari inayohitaji muda, uvumilivu, na mikakati sahihi. 

Maudhui unayotengeneza leo yanaweza kukupa wateja wengine miezi sita ijayo. Jaribu kuliangalia soko kwa mwaka unaokuja utakuwa katika hali gani. 

Ni muhimu kujua mchakato mzima wa masoko utakaoupitia na nini kinachohitajika ili kufikia malengo yako ya kuuza mtandaoni kwa urahisi. 

Licha ya kuwa idadi ya followers ni muhimu, inapaswa kuwa na lengo la kujenga uhusiano wa muda mrefu na wateja kwanza ambao watahamasika kuja kununua bidhaa au huduma zako.

Mwisho

Kabla ya kurusha matangazo, ni vyema kuanza kwa kuwekeza muda na fedha katika kujenga brand awareness na community. 

Hii itahakikisha kwamba wanunuzi watakapokuwa tayari, tayari wamefahamu na kuamini brand yako, na wako tayari kuchukua hatua ya kununua. Mkakati huu wa hatua kwa hatua utaongeza uwezekano wa kupata matokeo ya kudumu, badala ya matokeo ya haraka yasiyo na msingi.

Mafanikio ya kweli kwenye masoko ya kidigitali hayaji bin vuu kwa usiku mmoja. Inahitaji uvumilivu na uwekezaji wa muda mrefu. 

Matokeo bora yanapatikana kwa kufuata hatua hizi muhimu na hatimaye utaona matokeo yanayodumu na yenye tija kwa biashara yako. 

LinkedIn ni Chuo: Umuhimu wa LinkedIn na LinkedIn Learning Katika Kujifunza. 

LinkedIn ni Chuo: Umuhimu wa LinkedIn na LinkedIn Learning Katika Kujifunza. 

LinkedIn ni chuo kilichosheheni walimu waliobobea kwenye fields zao. Ukiachana na kupost, ukitulia vizuri na ukaamua kujifunza kutoka kwa watu wengine, kuna vitu vingi utajifunza tofauti na mtu ambaye hayupo kabisa LinkedIn.

Kuna umuhimu mkubwa sana wa kutumia mtandao wa linkedIn mbali na kupost ama kutafuta kazi.

Wapo watu ambao yamkini hawajapata fursa yoyote lakini kuwepo kwao linkedin wamehamasika kubadili maisha na mitazamo yao kwa ujumla.

Binafsi SEO, personal branding na mambo ya marketing nimejifunza kupitia LinkedIn learning. Kuwepo linkedIn kumenisaidia sana katika career yangu.

Tuangalie umuhimu wa wewe kuwepo LinkedIn katika kujifunza.

1. Linkedin ni jukwaa la kujifunza na kukua kitaaluma.

LinkedIn ni tofauti na majukwaa mengine yalivyo. Hili jukwaa siyo tu la kuchapisha habari au kutafuta kazi; ni mahali pa kujenga connection, kunoa ujuzi, na kupata maarifa mapya kila siku.

Kupitia posts zako watu watakupongeza na kukuchallenge kuhusu taaluma yako jambo ambalo ni zuri katika kujifunza. Hii itakufungua ubongo ubadili mtazamo juu ya hicho unachokijua sasa.

Ukiona posts zako zinapata negative comment usiwaze sana ni mambo ya kawaida mtandaoni.

Pia LinkedIn inakupa uwezo wa kushirikiana na watu wenye ujuzi wa hali ya juu kitaaluma kukuzidi kwenye sekta mbalimbali, na kwa kusoma makala zao zenye kuelimisha unaongeza madini mapya yatakayokusaidia kukuza taaluma unayojishughulisha nayo. 

Cha kufanya chagua watu wako watano fuatilia makala zao kila siku, hudhuria event zao (virtual events), na shiriki kwenye posts zao hakika utaweza kufungua milango ya fursa nyingi ambazo huenda pengine usingezipata popote. 

2. Kujiendeleza kiujuzi kupitia linkedIn learning

LinkedIn pia ina sehemu muhimu sana inayoitwa LinkedIn Learning. Hiki ndicho kitu muhimu sana kwa kujifunza na ndiyo kitu kilinifanya niazimie kusema linkedin ni chuo. Iwe wewe ni mfanyabiashara, mhitimu, mfanyakazi au CEO, hii ni sehemu sawadata ya kujifunza maarifa mengi zaidi.

LinkedIn Learning ni jukwaa la mtandaoni lenye maelfu ya kozi zinazotolewa na wataalamu kutoka sehemu mbalimbali duniani. Uzuri wake ni kwamba kozi hizi zote zinatolewa bure kwa mwezi mmoja wa mwanzo. Jifunze jinsi ya kujiunga LinkedIn premium bure leo hii upate kufaidika na kozi zilizopo. 

Kupitia LinkedIn Learning, unaweza kujifunza kila kitu kutoka kwenye masuala ya teknolojia, biashara, uongozi, hadi kwenye ujuzi wa mawasiliano na usimamizi wa miradi. Faida kubwa ya kutumia LinkedIn Learning ni kwamba unaweza kujifunza kwa kasi yako mwenyewe, popote ulipo, na muda wowote.

3. Inakupa uhuru wa muda wa kujifunza. 

Hii inamaanisha kuwa hata kama una ratiba ngumu, bado unaweza kupata muda wa kuongeza maarifa na ujuzi mpya ambao utakuongezea thamani katika soko la ajira. Moja ya vitu vya kipekee kuhusu LinkedIn Learning ni kwamba kozi zake zimeundwa kwa namna ya kiutendaji. 

Badala ya kupata nadharia tu kama ilivyo chuoni, hapa unapata pia maarifa ya jinsi ya kutumia ujuzi huo katika hali halisi ya kazi ofisini kwako.

Hii inakusaidia si tu kujifunza bali pia kuwa na ujuzi unaohitajika kwenye nafasi yako ya kazi. Kwa mfano, kama unataka kuboresha ujuzi wako wa uongozi, unaweza kuchagua kozi zinazohusiana na uongozi na usimamizi, kisha ukajifunza mbinu mbalimbali zinazotumika kwenye mazingira halisi ya kikazi.

4. LinkedIn learning inatoa cheti kwa kila course. 

Zaidi ya hayo, unapomaliza kozi huko LinkedIn Learning unapewa cheti ambacho unaweza kuweka kwenye profile yako LinkedIn. Vyeti hivi vinaweza kuwa na uzito mkubwa, hasa unapojitambulisha kama mtu anayejali maendeleo ya kitaaluma na anayeendelea kujifunza kila mara.

Mfano ukiangalia profile yangu ya LinkedIn sehemu ya Certification and Licence utakuta kuna vyeti nilivyovipata linkedIn Learning nimeviambatanisha pale. Kwako vyeti hivyo vitaongeza mvuto wako kwa waajiri au wateja watarajiwa. 

Mwisho wa yote, LinkedIn Learning inathibitisha kwamba kujifunza hakuishii darasani pekee. Katika ulimwengu wa sasa wa kidigitali, ujuzi unapatikana popote, wakati wowote, na kupitia jukwaa kama LinkedIn, unaweza kufikia malengo yako ya kitaaluma na kuwa na mafanikio katika kazi na maisha yako kwa ujumla. 

Kwa hiyo, ikiwa unatafuta jukwaa la kujifunza, kuboresha ujuzi wako, na kuongeza thamani yako katika soko la ajira, LinkedIn Learning ni rasilimali muhimu sana ya kuchukua hatua hiyo.

Kitabu: Tengeneza LikedIn Profile Ili Upate Ajira au Wateja

Kitabu: Tengeneza LikedIn Profile Ili Upate Ajira au Wateja

NIKUULIZE SWALI: Unataka kuonekana au kuchukuliwa SERIOUS? Unataka kuonekana UNAJUA au uonekane beginner, mgeni na mshamba wa LinkedIn au mtandao wa X? 

Kitabu changu kinakuhusu kama umekuwa ukijitahidi kupost na kucomment lakini hadhi ya jina lako bado DHAIFU na hauwezi kuuza.

Kinakuhusu pia wewe graduate uliyeenda kule LinkedIn na kuandika vitu kama:

Graduate student ❌

Seeking Opportunities ❌

Attended xxx University ❌

Looking For New Opportunities ❌

Jobseeker ❌

Degree holder in banking and finance ❌

Kinakuhusu na wewe uliyejiwekea UFINYU wa FURSA kwa kukomaa na X pekee wakati WAAJIRI na WATEJA serious wamejaa LinkedIn. Kwanini uweke mayai yako yote kwenye kapu moja?

Kwanini ni MUHIMU Kuwa na LinkedIn au X Profile BORA na Yenye KUELEWEKA?

Fikiria wewe ni striker. Umetoka na mpira katikati ya uwanja. Umepiga chenga mabeki wote na sasa niwewe na golikipa. Golikipa naye anakuja unamla tobo. 

Watu washanyanyuka vitini. Sasa ni wewe kutia mpira nyavuni.

Unapiga mpira…Halafu…UNAKOSA!!! 

Juhudi na chenga zote umeshindwa kumalizia!

Hivi ndivyo inavyokuwa ukiwa na LinkedIn profile mbovu, iko nusunusu au ina makosa ya wazi wazi. Utakuwa UNAKOSA watu wa kukutilia maanani.

Utakuwa unapost na kukocomment sawa, lakini mteja/mwajiri akija kuangalia Profile yako anakuta huna mkakati wa kumfanya achukue final decision ambayo ni kununua au kukuajiri.

Kuanzia Banner, Headline, Featured, About, Experience na Skills —yote hiyo ni mikakati ya umaliziaji. Usipoweka sawa maeneo haya, utakuwa unakosa magoli ya wazi kabisa.

Ugeni na ushamba wa jukwaa siyo sifa. Kama ilivyo kwenye sheria, kutokujua is a weak excuse. Badilika!

FAIDA 6 Za Kuwa Na Profile Inayoeleweka LinkedIn:

  1. Inafanya watu wasikuchukulie poa.
  2. Inakufanya upandishe bei ya huduma zako.
  3. Inakimbiza wazinguaji na kukuletea watu walio serious kulipia huduma zako.
  4. Inapunguza kujieleza sana maana inamaliza yote.
  5. Profile inakutangaza masaa 24 hata ukiwa zako umelala.
  6. Inalipa UZITO Jina lako.

Ni wachache sana wana Profile zinazowafanya wastahili kutazamwa mara mbili. Achilia mbali kukaa akilini na kufuatiliwa mara kwa mara na watu. Nataka uwe miongoni mwa hawa wachache.

🎯 I’m the most followed Tanzanian marketer on LinkedIn na huwa ninaona jinsi wabongo vile we sell ourselves shot kule. Hakuna mtu atakuja kukutonya juu ya haya niliyoyaweka bayana na kuyasahihisha kwenye Mwongozo huu.

Chukua Mwongozo huu UONDOE aibu ndogo ndogo na kubwa zinazoshusha hadhi yako kwenye hadhara ya wateja na waajiri. 

Bei yake haitoshi hata kupata lunch pale mjini kati. Ni Tsh 14,900 tu.

Bofya HAPA KUJIPATIA Nakala Yako Chap!

Ajira Ni Tatizo: Fanya Mambo Haya Ukiwa Chuoni

Ajira Ni Tatizo: Fanya Mambo Haya Ukiwa Chuoni

Changamoto kubwa inayosumbua vijana wengi ni tatizo la ajira. Kila sehemu utasikia ajira hakuna ila kazi zipo.

Umekuwa wimbo unaovunja rekodi kila siku kuanzia juu hadi ngazi ya familia.

Wimbo huu unaongoza kwa kuimbwa na wahitimu wengi wa vyuo hapa nchini na kuna wengine wamegeuza tatizo hili kuwa fursa. Jambo ambalo ni zuri.

Ukiwa chuo usikae tu kizembe jaribu kufanya mambo mbalimbali yatakayokusaidia kukwepa Unemployment baada ya kumaliza chuo. Ni bora kujiandaa mapema kuliko kusubiri hatima usiyoijua.

Kukabiliana na janga hili kuhusu mbinu gani utumie kutafuta kazi, kwanza inabidi ujiulize wewe kama mwanafunzi unataka kuwa nani? Mpaka sasa unafanya nini kuhakikisha unakuja kuwa huyo mtu?

Chukua kalamu na karatasi narudia chukua karamu na karatasi sasa hivi kaa pembeni peke yako anza kuandika what is the person you really want to be in the future na huwezi kufikiria sawa sawa upate majibu ya maswali haya kwa kusoma tu lazima uandike kwenye karatasi ndio unapata kutambua kwa ufasaha majibu ya maswali hayo.

Vijana wengi husema acha kwanza nimalize itajulikana mbele kwa mbele. Mbele ipi wakati ukimaliza chuo unaenda kwenu ambako kupata fedha ya vocha tu ni changamoto!

Hivi unafikiri ukimaliza chuo mambo yatanyooka kama unavyotarajia? hata wao walifikiri vivyo hivyo kilichotokea hawaamini hadi leo.

Haya hapa mambo matano (5) ya kufanya ukiwa chuoni

1. Chagua kitengo/somo moja utakaloteseka nalo hadi kumaliza chuo.

Ukiwa chuo huwezi kuwa vizuri kwa yale yote yanayofundishwa darasani na pengine usiyafanyie kazi kabisa maishani mwako japo ni vizuri kuyafahamu.

Ukiamua kusoma course fulani chagua kitengo kimoja tu utakachokuwa unasoma kila siku iwe mchana iwe usiku unakomaa nacho mpaka unamaliza chuo mfano ukiamua kuchakalika na network hakikisha network haikupigi chenga, pata taarifa zote zinazohusu network.

Kuanzia mwaka wa kwanza hadi mwaka wa mwisho unakomaa na network ama kwa hakika utakuwa vizuri sana baada ya kumaliza chuo kuliko yule anayehangaika na vyote leo yupo Business management kesho hacking kesho kutwa Software development. Wahenga walisema mtaka yote kwa pupa hukosa yote.

Komaa na kitu kimoja, hayo masomo mengine yasome kwa ajili ya kunawilisha cheti chako. Hapa naomba tuelewane kitu unachokisoma hakikisha unalijua soko lake vizuri siyo unakomaa na hiki mwisho wa siku unaishia kufanya vitu tofauti kabisa.

 

2. Anza kujitolea mapema.

Usisubiri mpaka umalize chuo ndio uanze kutafuta sehemu ya kujitolea. Chuo ndio sehemu nzuri ya kujitolea ikiwa bado unapata fedha ya kujikimu kuliko ile unamaliza chuo ndio unajitolea yaani hata ukipewa pesa kidogo inaishia kununua dagaa na usafiri.

Fanya ufanyavyo ili mradi upate sehemu uanze kujitolea, kipindi unamaliza chuo pengine waweza kuajiriwa kwenye hiyo hiyo taasisi au kampuni kwa kuwa utakuwa tayari unajua ABC kuhusu mambo yanavyofanyika.

Kuna majukwaa pia ya kidigitali ambayo unaweza kujitolea kwenye makampuni ya nje ikiwa bado uko chuo kama vile SkilledUp Life hapa utatengeneza profile yako na kuapply kazi kulingana na field yako.  

Kipindi wenzako wanahangaika kutafuta kazi wewe utakuwa unahangaika kupanga mafaili. Ukijitolea mapema utapata uzoefu mapema utakaokusaidia baadae kujibu lile swali liuzwalo kwenye chumba cha usaili “una uzoefu wa miaka mingapi”.

3. Noa ujuzi wako kila siku.

Usitegemee tu kile unachofundishwa darasani. Mwanafunzi mzuri ni yule anayetaka kujua nyuma ya pazia pakoje.

Siku hizi kuna majukwaa mengi yatoayo kozi za bure na za kulipia mtandaoni ni wewe na bundle lako tu mfano YouTube hapa kuna kila aina ya kozi unayotaka kujifunza, kuna kila suluhu ya matatizo unayoyapitia.

Pia kuna LinkedIn Learning (Free & premium) na HubSpot Free Courses. Kozi zingine za bure uki-search tu google wanakuletea. Ujue kuna watu wengine wamejiajiri kwa kunoa juzi zao kupitia majukwaa haya haya! 

Usiseme huna bundle mbona ukiingia Insta au Tiktok unamaliza masaa mawili na ushee kutizama short videos? Bundle unalo sema bado hujaamua kuwa serious hebu kuwa serious uone kama utakosa pesa ya bundle.

Kama unataka kupata kubali kupoteza. Hakuna kitu cha bure duniani lazima ulipie.

4. Ishi Maisha yako.

Chuo kuna changamoto moja. Kila kijana anataka aonekane yeye ndio yeye si mtoto wa mkulima si mtoto wa Waziri si mtoto wa mfugaji wote wanataka kuishi maisha sawa.

Mwingine akipiga simu nyumbani laki mbili kwake ni pesa ya chai wakati kwako ni pesa ya kula miezi miwili hapo unalipa na kodi kabisa.

Lakini ukiwa chuo unataka uishi maisha sawa na wao. Fanya ujikubali, usiishi maisha ya kuigiza kumbuka maisha siyo kuigiza, fuata kilichokupeleka chuo hao marafiki unaoshinda nao leo siku mkimaliza chuo kila mtu ataenda kwao na wewe utaenda kwenu.

Kama huamini subiri mmalize chuo. Ukimpigia mwenzako atakwambia yuko ofisini utampigia baadae wakati wewe upo huko ndani ndani kwenye shamba la ndizi – Itaba.

Kama serikali inakulipia ada na umebahatika kupewa pesa ya kujikimu (BOOM) itumie vizuri pengine inaweza kukusaidia huko mbeleni.

5. Chagua marafiki wa kuishi nao.

Bwana mmoja alisema nikitaka kukujua wewe ni nani na mwelekeo wako ni upi nionyeshe marafiki zako watano. Nikiwaangalia marafiki zako basi nitapat kukujua wewe ni nani.

Kama wanapenda mitoko na wewe utakuwa nusu yake, kama wanapenda kusoma na wewe ni nusu yake, kama wanafanya biashara na wewe ni nusu yake, kama wanapenda kucheza PS na wewe ni nusu yake. 

Hebu angalia marafiki ulionao kwa sasa na mambo wanayoyafanya halafu angalia na yako kama yanatofautiana sana.

Kuwa na marafiki ambao hawaendi njia unayotaka Kwenda ni sawa na kujichimbia shimo la kujilaumu baadae.

Bora ujiengue mapema na haimaanisha uachane nao kabisa. Hapana.

Jiweke kando na fanya mambo kivyako vyako mkikutana sehemu bongeni kama hakuna lililotokea huku ukiwa na moja kichwani. Ukitaka kujua zaidi kasome kile kitabu cha ATOMIC HABIT by James Clear utaelewa zaidi ninachokwambia hapa.

Hao jamaa zako usiwachukie wala kujiona wewe ndio mwamba wa Lusaka, maisha siyo hivyo ishi nao kwa akili mana hao rafiki zako ndio wanaweza kukuletea michongo mingi endapo utakuwa na ujuzi zaidi kuwazidi wao.

Maisha ni watu ishi nao vizuri.

Chuo ni daraja tu unapita tumia muda mwingi kuifikirie sana kesho kuliko leo yako. Nimalize kwa kusema hakuna anayeijua kesho maisha yako yapo mikononi mwako.