Ifahamu LinkedIn na Jinsi ya Kutengeneza Profile Itakayokupatia Fursa

Ifahamu LinkedIn na Jinsi ya Kutengeneza Profile Itakayokupatia Fursa

Linkedin ni mtandao wa kidigitali ambao unaunganisha watu wa kila aina kutoka pande zote za dunia hasa vijana wanaotafuta kazi, wajasiriamali wanaotaka kukuza biashara zao, kuboresha kazi zao na makampuni yanayotafuta wafanyakazi nayo pia yapo Linkedin.

Unaweza kuchukulia masihara ila wataalamu wengi wako kule yakiwemo makampuni, kule watu waliotengeneza jina wanaingiza pesa bila hata kwenda ofisini kuomba kazi, wengi wanafanya kazi kama freelancer.

Jinsi ya kujiunga linkedin

Kuna namna mbili za kujiunga linkedin, namna ya kwanza ni kusanikisha/kuinstall linkedin app kupitia playstore.  Andika Linkedin app kwenye search bar bonyeza iyo application ya blue kisha install. Baada ya kuinstall endelea na usajili, Linkedin app itaonekana kama hapo chini.

Namna nyingine ni kujisajili kupitia website ya linkedin, bonyeza Linkedin signup jaza taaarifa zinazohitajika, kuwa na kumbukumbu juu ya taarifa unazoziweka ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza baadae kama utasahau neon siri.


Sasa tumeweza kujiunga na kusign in, Linkedin watakutumia ujumbe kwenye email yako ili kuthibitisha kama gmail yako iko active, kinachofuata ni kumalizia usajili kwa kujaza taarifa zako ipasavyo kwani hizo taarifa ndizo zitakazokaa kwenye profile yako ya Linkedin

Tayari Tumeshatengeneza Akaunti, Sasa Twende Tukaifanye Profile Yako Iwe ya Kitaalamu.

Awali ya yote Linkedin siyo facebook, huku kidogo inabidi ujiweke katika mazingira mazuri uonekana as a professional, huku ndiko wateja wako walipo na ndiko utakapopata fursa mbalimbali za kukutana na watu, kushare idea, kubadilishana mawazo na watu mbalimbali kulingana na tasnia uliyopo.

Bila kupoteza wakati haya ni mambo muhimu inabidi uyafanye ili kuboresha profile yako.

1.Profile picture.

Hakikisha picha unayoweka kwenye profile inakutambulisha kama mtaalamu kwenye tasnia yako. siyo unapiga selfie ndio unatuwekea kwenye profile, Recruiters, wateja watakuona hauko serious. Picha hiyo iwe karibu na kamera, ionekane vizuri. Picha yako ndiyo utambulisho wako.

2. Banner.

Hapa utaweka background picture, texts au quote inayoendana na fani yako. Size ya background image huwa ni 1128 x 191. Wengine pia huweka namba zao za simu na email. Ni vizuri ukachagua kipi kinafaa uweke kuliko kuacha blank. Angalia mfano hapa chini.

3. Kichwa cha profile yako.

Hapa nazungumzia jina lako kamili na headline title ambayo itaonekana mwanzoni kabisa mwa profile yako. Hakikisha headline inajibu wewe ni nani, unasaidia nini?

Kufanikisha hili angalia hapo juu kushoto kuna kitufe kama kalamu bonyeza hicho na jaza taarifa zinazohitajika. Mfano Headline* yangu ni Built my brand while in college from 500+ to 7k people. Helping you do the same. Web developer & designer | Content Writer.

4. Kazi na Elimu.

Ili kuifanya profile yako inawili vizuri, hapo hapo kwenye profile kuna sehemu imeandikwa Open to work bonyeza hicho kipenseli, halafu weka cheo cha kazi unayofanya (job title) n.k 

Ukishafika kwenye visibility ruhusu recruiters only, hiyo nyingine siyo nzuri kuitumia kama kweli wewe unataka uonekane mtaalamu katika tasnia yako.

5. Experience/uzoefu

Pia utashuka chini kwenye Experience, hapo utaweka shule, makampuni au taasisi ambazo umeshawahi kufanyanayo kazi. Elezea kwa kiasi gani umeshiriki katika kuongeza ujuzi wako, vitu gani ulifanya n.k.

6. About

Hapa inatakiwa uelezee fani yako japo kwa kifupi, weka bayana nafasi uliyopo kwa sasa, unafanya nini, unatatua changamoto zipi, kwa namna gani, uzoefu wako ni upi kisha unaweka vitu ambavyo unaweza kuwasaidia watu wengine. Angalau ianzie aya mbili.

7. Mpangilio/Setting.

Mkono wa kulia juu kwenye profile yako kuna ikoni ya setting, ibonyeze shuka chini kidogo showing profile photo ruhusu kwa linkedin members wote. 

8. Usisahau kuwasha creator mode.

Hapa utaweka vitu utakavyokuwa unaongelea katika machapisho yako ya kila siku. Kwa kufanya hivi naamini kwa asilimia 90 profile yako itaonekana bora na ya kiprofessional zaidi.

Tumalizie, Linkedin pia inatoa fursa ya kujifunza course mbalimbali bure ndani ya mwezi mmoja. Je unapataje ofa hii?

 Ni rahisi tu, pale unapoingia linkedin home page kwa juu mkono wa kushoto kunaonekana profile picture yako, ibonyeze halafu angalia chini wameandika activate premium, pabonyeze halafu endelea na maelekezo. 

Baada ya hapo unaweza kujiunga linkedin learning ukapiga course mbali mbali ukishamaliza unapewa na cheti kabisa, ni wewe tu kufanya maamuzi leo. 

Muhimu: Kuwa makini kwenye Akaunti utakayotumia kwenye premium kama unaona siyo vizuri kutumia kadi yako ya bank unaweza kutengeneza M-Pesa VISA Card bure ndani ya dakika moja.

Baada ya kufanya hivyo inabaki kazi ya kujimwanga kwenye jukwaa kuwakilisha kile ulicho nacho hapa naongelea kupost, kushiriki kwenye mazungumzo na jumuiya ya Linkedin, kuendelea kuwa hai. 

Jinsi AI Inavyoweza Kutumia Sauti Yako Kuzungumza na Mtu Mwingine

Jinsi AI Inavyoweza Kutumia Sauti Yako Kuzungumza na Mtu Mwingine

Baada ya Yombo kusikia neno AI linatamkwa sana huku mtaani ikabidi  amuulize jamaa yake Kadozo ili apate kujua zaidi. 

Hivi ndivyo Mazungumzo yalivyokuwa.

(Kadozo na Yombo ni vijana wanaosoma chuo, BBM)

Yombo: Je, unafahamu chochote kuhusu teknolojia ya AI?

Kadozo: Ndiyo, na nimekuwa nikisoma vizuri kuhusu maendeleo ya kuvutia yanayoletwa na AI, kama ulishawahi kusoma the discovery of fire basi hii ni discovery of AI.

Labda kabla hatujaendelea nikuulize, hivi unajua kwamba AI sasa inaweza kutumia sauti yako kuanzisha mazungumzo na mtu mwingine?

Yombo: Hapana? Mbona hii ni ya kushangaza! Inakuwaje na Inafanyaje kazi?

Kadozo: Vizuri, mifumo ya AI inaweza kuchambua, kuiga sauti ya binadamu au rekodi za sauti ili kuunda mfano wa sauti itayotumika na AI.

Mfano, sauti hii ninayoitoa kama itarekodiwa, AI inaweza kukopi na kutumia sauti hii hii kuzalisha maneno yaliyosanifishwa ambayo katika kuongewa kwake yatafanana sana na sauti yangu.

Yombo: Oooh! Very interesting, Lakini inaanzishaje mazungumzo na mtu mwingine?

Kadozo: Mara tu AI inapokuwa imesanifisha sauti, inaweza kutumia algorithms za usindikaji wa lugha asili kuchambua na kuelewa maudhui ya mazungumzo yenu kisha kuzalisha majibu yanayofaa na kushiriki katika mazungumzo na mtu mwingine. Yaani kama AI itaanza kwa kusema hello! na wewe ukajibu-

Hapo ndipo mazungumzo yanapoanzia kwa sababu itakuwa inajibu na kuuliza maswali kulingana na majibu yako. Kumbuka hapa itatumika tu kama imetengenezwa kwa lengo la kuongea na mtu mwingine.

Cha kuongezea tu ni kwamba ni kivipi sauti yako inaweza kuchukuliwa na AI?

Moja kati ya njia ni kutumia kumbukumbu za sauti yako iliyonakiliwa awali, kama vile sauti zilizorekodiwa za mahojiano au hotubaKisha, AI inatumia teknolojia ya kujifunza ili kujenga mfano wa sauti yako na kuitumia.

Moja ya njia zinazotumika kurekodi sauti yako ni voice cloning . Njia nyingine ni kutumia sauti yako inayopatikana kwenye mitandao ya kijamii.

Kadozo: Kwa hivyo, AI inaweza kimsingi kutumia sauti ya mtu na kuwa na mazungumzo yenye maana na watu wengine?

Kadozo: Ndio, hilo halina ubishi. Unaambiwa huwezi kumnasa samaki aliyefumba mdomo kwa kutumia ndoano.

Kwa hiyo AI inaweza kusikiliza kile mtu anasema, kuiga habari hiyo na kujibu kwa njia ambayo inasimulika kama mazungumzo yanayofanana na ya binadamu.

Yombo: Duh! hii mpya, Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Napata kujiuliza maswali mengi sana ya usalama?

Kadozo: Maswali gani hayo tena Mr. Yombo?

Yombo:  Sasa kama ni hivyo mfano si AI inaweza kutumiwa ili kupata taarifa zangu binafsi za shule kama itaiga sauti ya registration officer?

Kadozo: Bila shaka. Matumizi ya AI kufananisha sauti ya mtu yanazua wasiwasi kuhusu faragha, wizi wa utambulisho, na matumizi mabaya ya habari binafsi.

Lakini nikwambie kwamba katika ulimwengu tuliopo usimwamini mtu yeyote anayehitaji taarifa zako, pia tumia “multifactor authentication” ili kama humwelewi umwambie atumie njia ya pili kuwasiliana na wewe.

Kwa kawaida AI ukiiuliza wewe ni ni nani itasema Mimi ni kompyuta program niliyeundwa blablaa.

Hapa chini tulipata kumuuliza ChatGPT na alitoa majibu yafuatayo.

Sasa karibia kila aina ya AI huweza kujitabulisha kulingana na ilivyopangiliwa. Hapa ni rahisi sana kujua kumbe unaongea na AI. 

Mfano, Assume ChatGPT ingebatizwa kwa jina lako la Yombo, hapo juu ingesema “Mimi ni Yombo blablaa” chukulia ndiyo unaongea nayo kwenye simu, hapo si ni rahisi kuamini unaye ongea nae ndiye bwana Yombo? Hivyo ndivyo mambo yanavyoenenda ndugu yangu.

Tunaishi katika wakati ambapo teknolojia inabadilika kwa kasi, na AI inachukua jukumu kubwa katika mapinduzi hayo. Lazima tuwe wazi na tayari kukabiliana na changamoto na masuala mengine yanayoweza kujitokeza.

Yombo:  Hiyo ni uhakika. Nashukuru sana ndugu yangu kwa kunitoa gizani, siku nyingine nitakutafuta tuangazie mambo mengine kwa undani zaidi.

Kadozo: Haina noma mshikaji wangu.

Unaweza ukawa unajua kuwa watu wote wanajua kumbe hawajui. Kama una swali lolote dondosha coment yako hapo chini utajibiwa.

Mbinu Mpya Ya Kupata Kazi Ukihitimu Chuo

Mbinu Mpya Ya Kupata Kazi Ukihitimu Chuo

Soko la ajira ni changamoto kubwa inayosumbua vichwa vya wanafunzi wengi hasa wale wanaohitimu vyuo vikuu katika nyakati hizi. Jambo ambalo linafanya vijana wengi wakose imani ya kufanikiwa tena.

Kwanza ijulikane kuwa degree peke yake sio kigezo cha mhitimu kupata kazi kwa sababu wengi huamini akimaliza chuo kazi ni yake. Sasa hivi bila kujiandaa mapema mambo ni magumu sana, soko la ajira ni gumu.

Hata hivyo, kupenya kwenye soko la ajira ni jambo linalohitaji juhudi, ujuzi na utayari wa mtu mwenyewe. Katika makala hii, tutaangazia jinsi mwanachuo anavyoweza kupenyeza kwenye soko la ajira.

Je, ni nini unachoweza kufanya kama mwanachuo ili kuongeza uwezekano wa kupata kazi?

Mchakato wa kutafuta kazi unapaswa uanze mapema, hata kabla ya kuhitimu. Je wewe ni mwanachuo?

Kama jibu ni Ndiyo, basi unaweza kuanza kutafuta fursa za kazi mapema mtandaoni au kwa kushiriki katika programu, miradi, semina, kuandaa projects na kujitolea katika makampuni.

Kwa kushiriki na watu wengine utapata kuongeza marafiki wapya (connection) ambao baadae wanaweza kuwa ndio daraja lako la kupata kazi.

Pia ukianza kujitolea mapema ukiwa chuo utapata uzoefu wa kazi mapema through internship/freelancing ambao utakusaidia kuwa na ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira pindi tu umalizapo chuo.

Ivi ulishawahi kusikia au kuulizwa hili swali, unauzoefu wa miaka mingapi? chukulia ndio tu umemaliza chuo halafu unaingia interview kuulizwa hilo swali, utajibu nini? Hivyo anza mapema kutafuta makampuni ujitolee au ufanye freelancing ili baadae swali hili lisikusumbue.

Ni nini kinachotarajiwa kutoka kwako katika soko la ajira?

Unaweza kujenga mtandao wako wa kijamii (networking) kwa kuwa na mahusiano mazuri na walimu, wanafunzi wenzako na wataalamu wa tasnia yako. Kupitia mtandao huu, utaweza kupata taarifa za kazi pale zinapopatikana.

Hapa nina maanisha uwe na watu ambao watakuwa wana-support kile unachokifanya. Ukiishi na watu ambao hawasupport unachokifanya maana yake hakuna kazi utapata kupitia wao.

Muhimu: Kwa dunia tuliyopo, kama mwanachuo ataamua kuitumia vizuri mitandao ya kijamii yaani social media platforms kama Linkedin katika kujiuza (personal branding) basi mtu huyu;

Hatakuwa anatafuta kazi bali kazi zitakuwa zinamtafuta yeye by Shukuru Amos.

Soko linahitaji vijana wenye maarifa ya kufanya kazi fulani, kuna kazi zingine hata hazihitaji cheti kikubwa uwe na uwezo wa kutatua changamoto za kampuni husika au uwezo wa kuisadia kampuni ikaongeza mauzo au kupandisha hadhi yake?

Jinsi gani unaweza kuboresha ujuzi wako, kupata maarifa yanayohitajika katika tasnia uliyopo?

Technolojia inabadilika kwa kasi sana hivyo unaweza kutumia mitandao ya kijamii kufuatilia mabadiliko yanayotokea katika tasnia yako na kujifunza ujuzi mpya kupitia kozi mbalimbali mtandaoni ikiwemo Marketing.

Chuoni utapewa Mwongozo tu hivyo kuna kila sababu za kutafuta maarifa zaidi. “Kama elimu ya chuo itashindwa kukufanya kuwa unachotaka basi Professor Youtube na msaidizi wake Google wanaweza”.

Utajiuliza ni kivipi Youtube au google inaweza kukusaidia kutimiza ndoto zako? Unahitaji tu kujua unataka usome nini then weka bundle YouTube anakufungulia dunia kuwa unachotaka.

Je ni sahihi kuweka wasifu wako mtandaoni?

Kutengeneza wasifu wako mtandaoni kunaweza kukusaidia sana katika harakati za kutafuta kazi. Wasifu huo utakuwa hewani 24/7 unasomwa na watu wa aina tofauti tofauti ikiwemo waajiri wako baadae, wateja wako.

Hivyo ni vyema kuweka mawasiliano yako, barua pepe na nambari ya simu katika kurasa zako ili watu wakikuhitaji iwe rahisi kukupata.

Wasifu wako mtandaoni unaweza kuwa fursa nzuri kwa wateja au waajiri wanaotafuta talents mtandaoni kujua zaidi kuhusu wewe, uwezo wako na kitu unachoweza kuwasaidia.

Iwe ni Twiter, Facebook, au LinkedIn we jiweke as a professional wa kitu fulani huwezi kujua huko mbeleni ni fursa gani unaweza kuipata. Who knows what will happen tomorrow?

Nifanye nini ili nitambulike na niweze kupata kazi?

Kujitangaza ni muhimu sana katika ulimwengu wa kidigitali hasa unapokuwa kwenye harakati za kutafuta kazi.

Wewe Mwanachuo unapaswa kuwa na ujuzi wa kujielezea mwenyewe katika majukwaa ya aina yoyote iwe kwa maandishi au kwa kuongea.

Kujifunza jinsi ya kuwa mbele kiujuzi na kimaarifa kunaweza kukusaidia kuwa na ujasiri, uwezo wa kuwasilisha mawazo, kushawishi waajiri wakupe kazi.

Asilimia 90 ya mazungumzo mtandaoni huwa ni kwenye maandishi hivyo ni bora kuwa vizuri zaidi kwenye uandishi.

Bonus: Mtu awaye yote, mwenye kutafuta afueni ya maisha yake, yambidi afanye bidii na juhudi zote katika kutatua matatizo yanayoisibu tasnia yake.

Je, ChatGPT Inaweza Kudukua Taarifa Zako?

Je, ChatGPT Inaweza Kudukua Taarifa Zako?

Hapana. ChatGPT haiwezi kudukua taarifa za watumiaji wake. Zana hii ya AI (Artficial Intelligent) ipo kwa lengo la kukusaidia kufanya kazi zako kama vile kuandaa maudhui kwa uharaka na ufanisi mkubwa.  

Pia ChatGPT, amabaye kimsing ni roboti unayeweza kufanya mazungumzo naye, anaweza kukupatia majibu ya maswali yako yoyote utakyouliza.

Hizo ndizo kazi za ChatGPT. Siyo kukusanya au kudukua taarifa zako.

Kama ulishawahi kutumia ChatGPT utajiuliza kwanini upande wa kushoto mwa smartphone au desktop yako ukiwa ume-login huwa kuna record za maswali yote uliyokwisha kumuuliza ChatGPT?  

Ni kwamba mazugumuzo yote ambayo unafanya na ChatGPT hurekodiwa kwenye (hifadhidata) database ya OpenAI. Hii inakuwezesha wewe kuweza kuona mambo yote uliyowahi kuchati naye. Lakini pia inakupa option ya Ku-delete kama huhitaji mazungumzo yaendelee tena kuligana na mada uliyokuwa unachat naye.

Pia huisaidia ChatGPT kukumbuka nini mnazungumzia hasa mazungumzo yakiwa ni endelevu.  Hapo tunapata hili Swali hapa chini:

Endapo hifadhidata ya OpenAI itakuwa-attacked, je, taarifa za mtu zinaweza kudukuliwa?

Hilo liko wazi; kama uliwahi kutoa taarifa zako binafsi (sensitive data) kwa ChatGPT basi hautakuwa katika mikono salama tena katika kipindi ambacho hifadhidata ya OpenAI itakuwa attacked.

Steve Mills, mtaalamu wa masuala yahusuyo AI na Maadili anasema “then you have lost control of that data and somebody else have it.” Ndio maana unaambiwa usimshirikishe ChatGPT taarifa zako binafsi.

Fuatilia katika hii link https://www.openai.com/blog/march-20-chatgpt-outage

Je, matumizi ya ChatGPT yanaweza kusababisha kuvuja kwa taarifa za kampuni?

Ndiyo, kama kuna mmoja kati ya wafanya kazi katika kampuni anatumia ChatGPT katika shughuli zake na kwa namna moja ama nyingine alihusisha au huhusisha taarifa nyeti za kampuni pindi akiwa anawasiliana na ChatGPT, Mtu huyu anaweza kusababisha security breaches of the network endapo tu akaunti yake ya ChatGPT itakuwa hashed/known na kuwapa uwanda mpana watu wengine kupata network datails alizoshare na ChatGPT akiwa anachat.

Hapa kwenye hashing itategemeana na urefu, ugumu wa nenosiri, kifaa anachotumia n.k.  Kumbuka hapo pia kuna Man in the middle attack.

Samsung waliliona hili na hivyo kuzuia wafanyakazi wake wasitumia generative AI kama ChatGPT ili kulinda usalama wa kampuni.