Jinsi Ya Kumsaidia Mjasiriamali Mdogo Kukuza Biashara Yake Mtandaoni

lady looking on her ipad

Written by Shukuru Amos

I am the founder of Tanzlite Digital, Creator, Author of Mbele Ya Muda, and the most followed Tanzanian marketer on LinkedIn.
๎€ฃ

Posted November 11, 2020

Hakuna mtu ambaye anaweza kufanikisha jambo bila msaada wa mtu au watu wengine. Tunaishi kwa kutegemeana. Unachokitafuta wewe kipo kwa mtu mwingine.

Katika dunia yetu ya kidigitali, ni rahisi kuwa sehemu ya msaada mkubwa kwa wajasiriamali wanaotafuta kukuza biashara zao mtandaoni. Unaweza kufanya hivyo bila hata ya kutumia pesa.

Jinsi ya kusaidia kukuza biashara ya mjasiriamali mtandaoni

Follow page yake ya biashara. Inaweza kuwa ni instagram, twitter au facebook – popote unapoona unaweza kumfolllow fanya hivyo. Hii haigarimu pesa yoyote.

Toa Comment , Like au Share post za bidhaa zake ili zipate kuonekana kwa wengi. Kumbuka wewe binafsi una followers ambao nao wana followers, hivyo ukishare au kucomment kweny post ya mjasiriamali huyu, unaipa nafasi post yake kufika mbali zaidi. Hii nayo haikugarimu hela.

Toa maoni, reviews auratings kuhusu huduma yake kwenye page yake Google My Business, kwenye App yake playstore, au kwenye listing directories zingine.

Weka picha ya eneo au bidhaa yake na shiriki kuhakiki (verify) taarifa zake kwenye ramani za google.

Pia wajuze marafiki zako juu ya bidhaa zake.

Cha mwisho, acha kuponda biashara ya mtu mtandaoni. Kama kuna kitu unaona anakosea ni busara kumtumia ujumbe inbox na kumweleza.

Ukifanya yote haya, utakuwa umetumia kiasi cha shilingi SIFURI!

Lakini utakua umemwezesha mtu kufikisha bidhaa yake kwa walengwa hivyo kujipatia kipato cha kuendesha maisha yake. Si lazima uwe na pesa kusaidia, japo ni vizuri zaidi kutoa ukiwa na uwezo huo.

Kama somo limeeleweka, naomba follow page za Tanzlite Digital kwenye mtandao wa LinkedIn, Facebook, Twitter na Instagram. Pia nenda kafanye hivo kwenye biashara ya mjasiriamali unayemjua.

Kugusa maisha ya watu wengine si lazima uwe Bill Gates. Kusaidia kukuza online visibility ya biashara ya mtu ni aina nyingine ya philanthropy!. Tuendelee kuinuana. Usisahau kushare post hii ๐Ÿ™‚

Natumaini makala hii imekusaidia. Naitwa Shukuru, ni mwandishi na mtaalamu wa Digital Marketing. Nipate kupitia mtandao wa WhatsApp hapa.

2 Comments

  1. Claud John

    I need book which help to grow my business

    Reply
    • Shukuru Amos

      Habari Claud, Kitabu changu cha Mbele Ya Muda kitakupa maarifa juu ya Biashara MtandaonI; jinsi ya kuandaa maudhui ya kuvutia wateja pamoja na kukuza jina binafsi wewe kama mmiliki wa biashara yako. Bofya Hapa Kupata kitabu.

      Reply

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Governments vs Social Media: Build That Website

Governments vs Social Media: Build That Website

It is not a wise idea to put all your eggs in one basket. Especially if you have little ownership of that basket. Recent feuds between governments and social media giants highlight the risks of relying on third-party platforms for business. Hereโ€™s why owning your...

Introducing Tanzlite Host: The New Web Hosting Player in Tanzania

Introducing Tanzlite Host: The New Web Hosting Player in Tanzania

Earlier this year, we introduced Tanzlite Host. This is not just another name in Tanzania's web hosting services; we're rewriting the rules. Here's how our unique approach to business is setting us apart and why it's the most profitable model in the industry: A...

Products From Tanzlite