Habari kwa Digital Writers Tanzania. Sasa Unaweza kujipatia pesa kwa kuandika kwenye jukwaa la Medium. “We’ve added 77 countries to the Medium Partner Program” taarifa rasmi kutoka Medium ilisema mnamo August 6, 2024.
Kabla ya hapo, Tanzania haikuwemo miongoni mwa nchi ambazo writers waliweza kujipatia pesa kupitia makala zao kusomwa. In fact, hakukuwa na nchi hata moja ya Afrika.
Kama ilivyo kwa majukwaa mengine yanayolipa watengeneza maudhi, kuchelewa kwa Tanzania kuwa kwenye orodha ya Medium Parter Program ilitokana na shida ya njia ya malipo. Wanatumia Stripe kugawa malipo.
Mwezi Februari nilijaribu kujiunga nikaambiwa “You are located in a country that is not eligible for payouts.” Basi kwenye orodha hii mpya, Tanzania imo. Kazi kwako msaka maokoto mtandaoni.
Je Jukwaa la Medium ni Nini?
Mtandao wa Medium ni kama YouTube lakini kwa waandishi. Ni jukwaa la waandishi wa makala zinazohusu mada mbalimbali. Yaani unaweza kuandika chochote kwa ujuzi, uzoefu au maoni yako. Medium inakuwezesha kumiliki blog yako ambayo tayari ina wasomaji maana watumiaji wa jukwaa lile ni takribani milioni 100 kila mwezi.
Je Unalipwaje kwa Kandika Medium?
Kupitia Medium Partner Program, ukiandika makala yako ikapata engagement kama vile likes/claps, comments na activity zingine kama highlights, unaweza kujipatia kiasi fulani cha pesa (in dollars). Zikifika dollar 10, zitatumwa kwenye akaunti yako ya benki yoyote hapa Tanzania.
Masharti ya Kujiunga.
Ni lazima uwe mtumiaji wa Medium Pro, wenyewe wanaita kuwa Medium Member. Ni dola $5 kwa mwezi. Kama hauko tayari kutumia pesa ili upate pesa basi fursa hii si yako. Pia uwe umechapisha makala kwenye jukwaa hilo kwa kipindi cha ndani ya miezi 6 iliyopita. Hii maana yake: Unaweza kujiunga leo na ukaandika makala zako mbili au tatu hala ukaomba kujiunga kwenye programu ya kulipwa. Epuka kutumia AI kuandika makala zako, hiyo hawataki kabisa. Wanataka ubora na uhalisia.
Zaidi ya hapo hakuna masharti magumu. Unaweza soma zaidi hapa kufahamu Medium Partner Programu ni nini.
Je ni Nini cha Kuandika?
Andika chochote unachokijua, uzoefu wa maisha au ujuzi wako kitaaluma. Hakuna masharti ya nini cha kuandika. Ila ushauri tu kwako Mtanzania, andika kwa Kiingereza ili usijifunge kuandikia Waswahili tu.
Mimi binafsi ninaandika makala kwenye jukwaa la Medium. Unaweza kuni-Follow hapa.
0 Comments